January 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wahitimu 400 kupelekwa hospitali za rufaa

Hospitali ya Rufaa ya Bugando, iliyopo jijini Mwanza.

Spread the love

SERIKALI inakusudia kuwapeleka wahitimu wa sekta ya afya wapatao 400 katika hospitali za rufaa nchini. Anaandika Dany Tibason … (endelea).

Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Stephen Kebwe ameliambia Bunge wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalum, Diana Chilolo (CCM).

Katika swali lake, Chilolo aliitaka serikali kupeleka madaktari katika hospitali ya Ikungi kwa kuwa licha ya kupandishwa hadhi kuwa hospitali ya rufaa lakini haina wataalamu wa kutosha.

Dk. Kebwe amesema katika mpango wa serikali wa kuimarisha hospitali za rufaa za wilaya, mikoa na kanda kwa sasa inao wataalam zaidi ya 400 walio vyuoni na kwamba kwa kadri watakavyokuwa wanahitimu watapelekwa katika hospitali hizo.

Awali akijibu swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalum, Dk. Pudenciana Kikwembe (CCM), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi), Celina Kombani amesema Wilaya ya Mlele ilipewa maelekezo ya jinsi ya kufanya ili kituo cha afya Iyonga kipandishwe hadhi kuwa hospitali ya wilaya.

“Melekezo hayo ni pamoja na kuwa na jengo la upasuaji, jengo la kuhifadhi maiti, chomeo taka, jengo la maabara, chumba cha mionzi, kuweka mfumo wa maji safi na maji taka na kufunga mfumo wa umeme kwenye majengo yote ya kituo cha afya,” amesema.

Kwa mujibu wa Kombani, Halmashauri ya Wilaya ya Mlele imeanza utekelezaji kwa kuingia mkataba na SUMA JKT wa Sh. 16 bilioni 1.6 ili kukamilisha mapungufu hayo.

Amesema inatarajiwa ifikapo Septemba 2015, majengo hayo yatakuwa yamekamilika.

Katika swali lake, Dk.Kikwembe alitaka kujua lini kituo cha afya Iyonga kitapandisha hadhi na kuwa Hospitali ya Wilaya ya Mlele.

error: Content is protected !!