January 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wahindi wavuruga zoezi la usafi Mwanza

Spread the love

ZOEZI la usafi katika Jiji la Mwanza limeingia dosari baada ya Wananchi kutishia kugoma kufanya usafi, wakimtaka Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo, kuwaamuru watanzania wenye asilia ya kiasia waliokuwa wamejifungia ghorofani kushiriki kwenye shughuli hiyo. Anaandika Moses Mseti, Mwanza … (endelea).

Hali hiyo ilijitokeza jana baada ya wananchi waliokuwa wakifanya usafi katika eneo la soko kuu la Mwanza na barabara ya Reli, huku wenzao wenye asili ya kiasia wakiwa ghorofani wakichungulia kwa chini kitendo ambacho kiliwakasilisha.

Wananchi hao walidai kuwa kitendo cha wao kufanya usafi huku wenzao wakiwa ghorofani ni jambo la aibu kwani Watanzania wenye rangi nyeusi wamekuwa wakionekana kama wafanyakazi kwao hivyo kiongozi huyo anapaswa kuwachukulia hatua.

Hata hivyo wakati wananchi hao wakitoa malalamiko yao, baadhi ya watanzania hao wenye asili ya kiasia ambao walikuwa wakipita eneo hilo, walishinikizwa kufanya usafi baada ya kutishiwa kupigwa.

Mmoja wa Wananchi hao, Meshack Bandawe, amesema zoezi la usafi ambalo Rais John Magufuli, ameagiza kufanyika nchini kote inapaswa kutiliwa mkazo na kila mtanzania anapaswa kufanya usafi katika eneo lake.

Bandawe ambaye Pia ni Meneja wa Mfuko wa Pensheni Mkoa wa Mwanza, amesema suala hilo halipaswi kubezwa kwani ni suala linachogusa maisha ya binadamu litasaidia binadamu kuepukana na ugonjwa kipindupindu.

“Huu usafi unapaswa kuwa ni mwendelezo kwani magonjwa ya milipuko kama vile kipindupindu yatatoweka, lakini watu wengine utakuta wanabeza kufanya usafi,” amesema Bandawe.

Kaimu Meneja wa Benki ya Tanzania (BOT) Mkoa wa Mwanza, Mussa Mziya, amesema Serikali inapaswa kuhakikisha inatafuta vifaa vya kufanyia usafi vinakuwepo ili kujikinga na magonjwa mbali mbali ya milipuko.

Amesema endapo Serikali itafanya hivyo, zoezi hilo litakuwa linafanyika bila kuwepo changamoto yeyote kwani ulinzi wa afya na salama wa binadamu utakuwa umeimarishwa zaidi kitendo ambacho kitaleta tija kwenye Taifa.

Pia ameishauri Halmashauli ya Jiji la Mwanza na Tanzania kwa ujumla kuhakikisha wanasimamia sheria za usafi wa mazingira kwa kuwachukulia hatua wale wote wanaokiuka taratibu, kanuni na sheria hizo ili kulinda mazingira.

error: Content is protected !!