Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Wahariri Tanzania wawaonya wanasiasa
Habari Mchanganyiko

Wahariri Tanzania wawaonya wanasiasa

Deudatus Balile, Kaimu Mwenyekiti wa TEF
Spread the love

JUKWAA  la Wahariri Tanzania (TEF) limewataka wanasiasa nchini humo kutokutoa matamshi ya kuwachochea wananchi kujenga chuki dhidi ya wanahabari na vyombo vya habari hususani kipindi hiki cha kuelekea  Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma…(endelea

Kauli hiyo imetolewa jana Jumapili tarehe 23 Augost 2020 jijini Dodoma na Kaimu Mwenyekiti wa TEF, Deodatus Balile  alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wakati akihitimisha mkutano mkuu wa wahariri.

Balile alisema, wanasiasa wanatakiwa kuchunga kauli zao pindi wanapokuwa katika mikutano yao ya kisiasa na zaidi wajikite kunadi sera zao na kuwaelezea wananchi watafanya nini pindi watakapopewa ridhaa ya kuongoza.

“Jukwaa limelazimika kutoa tamko hilo kutokana na kauli iliyotolewa hivi karibuni na aliyekuwa mbunge wa jimbo la Iringa Mjini kupitia Chadema, Mchungaji Peter Msigwa kwa kuwahamasisha wananchi kuwapuuza waandishi na vyombo vya habari.”

Mch. Peter Msigwa, Mbunge wa Iringa Mjini

“Hivi karibuni kuna taarifa inatembea katika mitandao ya kijamii ikieleza Mchungaji Msigwa aliwahamasisha wanachama wa Chadema kuwa wawapuuze waandishi wa habari na vyombo vya habari kwa kuwa waandishi walisusa kuandika habari za Chadema wakati alipokuwepo mgombea urais wa Chadema Tundu Lissu wakati akitafuta wadhamini.”

Balile alisema, “kauli kama hizo zinaweza kusababisha chuki kwa wananchi na kama hatutakemea kauli hizo kuna siku viongozi wa siasa wanaweza kuhamasisha waandishi wapigwe na wakapigwa.

“Kwa maana hiyo, Jukwaa hatukatai waandishi wawe sehemu ya kupigwa kwani waandishi hawana vyama na wanatakiwa kufanya kazi zao kwa mujibu wa sheria na utaratibu kwa lengo la kuwahabarisha watu wote” amesema Balile.

Hata hivyo, Balile aliviasa vyama vya siasa kushirikiana na waandishi wa habari kwa kuwapa ratiba au taarifa pale wanapokuwa wakifanya mikutano kwani waandishi hawawezi kuwa wanatambua kinachofanyika kila mara kwakuwa wanahabari siyo wanasiasa.

Pamoja na mambo mengine, Balile alisema, taaluma ya habari  ni mhimiri wanne hiyo imethibitika katika kipindi chote cha ugonjwa wa Corona nchi ilikuwa ikiendeshwa na vyombo vya habari kwa kutoa elimu kwa jamii kwani kila mtu alikuwa akitumia vyombo vya habari na jamii iliweza kupata elimu hasa kutumia vifaa vilivyokuwa vikitakiwa kama vile vitakasa mikono na utumiaji wa maji tiririka.

Aidha Kiongozi huyo alisema, vyombo vya habari nchini vinatakiwa  kuzingatia kanuni, sheria, miongozo na maadili ya uandishi wa habari na kukataa kutumiwa na wanasiasa wenye ajenda zao binafsi ambazo hazina misingi ya Taifa.

 “Tunapoelekea katika uchaguzi mkuu, wanahabari tuhakikishe tunaitumia nguvu hiyo kwa uangalifu ili kuweza kujenga taifa letu kwa maana ya kwamba sisi hatuna nchi nyingine zaidi ya Tanzania” alisema Balile.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!