January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wahariri MwanaHALISI, MAWIO wahojiwa, wanyimwa dhamana

Spread the love

IKIWA ni siku mbili baada ya Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kuanza kuwasaka wahariri wa gazeti la MwanaHALISI na MAWIO, hatimaye leo wamejisalimisha na kuhojiwa kwa masaa nane. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).

Hatua ya wahariri hao kujisalimisha katika Kituo cha Kati cha Polisi kilichopo eneo la Stesheni ilitokana na kuwepo kwa taarifa za kutafutwa na jeshi hilo mara kadhaa kwenye ofisi zao zilizopo Kinondoni na Magomeni Mwembechai bila mafanikio.

Mhariri wa gazeti la MwanaHALISI linalochapishwa na Kampuni ya Hali Halisi, mhariri mkuu wake ni Jabir Idrissa ambapo gazeti la MAWIO linalochapishwa na Kampuni ya Victoria Media Service Ltd linasimamiwa na Simon Mkina.

Wahariri hao kwa pamoja wamefika kwenye kituo hicho saa 8:54 mchana huku wakiongozana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Hali Halisi, Saed Kubenea; wakili Frederick Kihwelu na Mhariri Mtendaji wa Gazeti la MwanaHALISI, Ansbert Ngurumo ili kupata taarifa zaidi juu ya kusakwa kwa wahariri hao.

Wahariri hao walihojiwa kwa zamu kwa masaa nane, kuanzia muda waliojisalimisha hadi saa tano usiku, lakini polisi hao waliwanyima dhamana na kuahidi kesho kuwafikisha mahakamani.

error: Content is protected !!