June 22, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Wahariri MAWIO, Lissu kortini

Spread the love

SIMON Mkina, Jabir Idrissa na Tundu Lissu kesho watapandishwa katika Mahakama ya Mkazi Kisutu kujibu mashtaka ya uchochezi, anaandika, Hamisi Mguta.

Mkina ni Mhariri wa Gazeti la MAWIO, Jabir Idrissa, Mhariri wa gazeti la MwanaHALISI pia mwandishi wa MAWIO na Tundu Lissu, Mwanasheria wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Ni baada ya Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kuthibitisha kuwa, litawafikisha mahakamani kwa madai ya kuandika habari za uchochezi.

Lissu ameunganishwa katika kesi hiyo kwa madai ya kutoa kauli za uchochezi zilizoandikwa kwenye gazeti hilo. Pia mchapishaji wa gazeti hilo naye atafikishwa mahakamani.

Pamoja na Gazeti la MAWIO kufungiwa Januari mwaka huu baada ya kudaiwa kuandika habari za uchochezi zilizohusu mgogogo wa kisiasa visiwani Zanzibar ikiwa na kichwa cha habari ‘Machafuko yaja Z’bar’ katika toleo lake la 182 la Januari 14-20, 2016, bado serikali inawang’ang’ania.

Akizungumza na wanahabari Mkina amelaumu kitendo cha polisi kukamata hadi watoa maoni wa gazeti.

Mkina amesema, serikali inabana uhuru wa habari pia kunyima fursa ya kuikosoa hata kama imefanya mabaya.

error: Content is protected !!