Friday , 3 February 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Wahariri kumsapoti Rais Mwinyi Uchumi wa Buluu
Habari Mchanganyiko

Wahariri kumsapoti Rais Mwinyi Uchumi wa Buluu

Spread the love

 

JUKWAA la Wahariri Tanzania (TEF), limeahidi kuunga mkono ajenda ya Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi, ya kuvifanya visiwa hivyo kuwa na uchumi wa buluu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea).

Ahadi hiyo imetolewa leo Jumatano, tarehe 9 Machi 2022 na Mwenyekiti wa TEF, Deodatus Balile, akizungumza katika mkutano wa sita wa jukwaa hilo, uliofanyika Kikwajuni, visiwani Zanzibar, ambapo mgeni rasmi ni Rais Mwinyi.

Mwenyekiti huyo wa TEF, amesema kauli mbiu ya mkutano huo ni ‘Uchumi wa Buluu na Mawasiliano ya Umma’, ambayo imechaguliwa ili kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais Mwingi.

“Mwaka huu kaulimbiu ni uchumi wa buluu na mawasiliano ya umma, tumeichagua kwa nia ya kuunga mkono juhudi unayofanya, katika ajenda ya uchumi wa buluu,” amesema Balile.

Balile amesema “tumefuatilia kwa karibu tangu ulivyoingia madarakani, Zanzibar iliyofahamika kama visiwa vya marashi ya karafuu, leo imepakwa rangi mpya inayong’aa midomo mwa watu na kinachozunguzmwa ni uchumi wa buluu.”

Balile amesema, juhudi za Rais Mwinyi katika utekelezaji wa sera ya uchumi wa buluu ni kuhakikisha uchumi wa Zanzibar unaimarika.

Amesema wahariri na waandishi wa habari, watatoa mchango mkubwa katika kufanikisha utekelezaji wake, kwa kuihamasisha jamii kushiriki, kwa kuandika habari zinazohusu uchumi wa buluu.

Deudatus Balile, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF)

“Tunafahamu uchumi wa buluu ni eneo jipya la uwekezaji, ambalo halijafahamika vyema kwa wananchi. Nia yetu kama whaariri ni kujielimisha kwanza katika eneo hili, kisha tufanye kazi ya kuielimisha jamii,” amesema Balile.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NMB yafadhili ziara ya mafunzo machinga, bodaboda Dar nchini Rwanda

Spread the loveBENKI ya NMB imefadhili ziara ya siku nne ya mafunzo...

ElimuHabari Mchanganyiko

Waliopata Division one St Anne Marie Academy waula, Waahidiwa kupelekwa Ngorongoro, Mikumi

Spread the love WANAFUNZI wa shule ya St Anne Marie Academy waliofanya...

Habari Mchanganyiko

Wadau wataka kasi iongezeke marekebisho sheria za habari

Spread the love  WADAU wa tasnia ya habari wametakiwa kuongeza juhudi katika...

Habari Mchanganyiko

TEF yawatuliza wadau wa habari marekebisho vifungu kandamizi

Spread the love  JUKWAA la Wahariri Tanzania (TEF), limewataka wadau wa habari...

error: Content is protected !!