March 8, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Waharibifu wa miundombinu Mbeya wafikishwa mahakamani

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, SACP Ulrich Matei

Spread the love

JESHI la Polisi mkoa wa Mbeya limewafikisha mahakamani watu nane ambao ni wanakijiji cha Ngole kwa tuhuma za kufanya uharibifu wa mabomba na vyanzo vya maji vya kijiji hicho kwa kutumia silaha za jadi na kusababisha hasara ya Sh. 14 milioni. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Akizungumza na wanahabari leo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, SACP Ulrich Matei amesema watuhumiwa hao wamefikishwa katika Makama ya Hakimu Mkazi jijini Mbeya tarehe 21 Agosti, 2018 na kufunguliwa kesi ya uhujumu uchumi kesi namba ECO/13/2018.

Kamanda Matei amesema kuwa, watuhumiwa hao ambao ni Bosco Tayari (55), Damas Richard (25), Hadi Mwinuka (38), Nicolas Aman (20), Elia Jackson (50), Majuto Mussa (22), Andrew Jackson (19) na Elda Zabron (19), wako gerezani hadi tarehe 5 Septemba mwaka huu pale kesi hiyo itakapotajwa tena na mahakama.

Watuhumiwa hao mnamo tarehe 14 Agosti, 2018 kuanzia majira ya saa 10:00 asubuhi katika Kijiji cha Ngole, Kata ya Ilungu, Tarafa ya Tembela, Wilaya ya Mbeya Vijijini, wanadaiwa kwa makusudi na bila halali waliharibu mabomba na vyanzo vya maji kwa kutumia silaha za jadi na kusababisha hasara ya takribani Sh. 14 milioni mali ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwa ni michango ya baadhi ya wanakijiji na wafadhili.

error: Content is protected !!