April 14, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Wagonjwa wa corona Tanzania waongezeka

Spread the love

IDADI ya wagonjwa wa Homa Kali ya Mapafu inayosababishwa na  Virusi vya Corona (COVID-19), nchini Tanzania wamefika 19. Inaripoti Regina Mkonde…(endelea).

Taarifa hiyo imetolewa leo tarehe 30 Machi 2020 na Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

Waziri Ummy amesema, wagonjwa watano wapya, watatu wanatoka jijini Dar es Salaam na wawili wanatoka visiwani Zanzibar.

“Ninapenda kutoa taarifa kwamba leo tumethibitisha kuwepo kwa wagonjwa wapya watano wa COVID-19, baada ya kufanyiwa vipimo katika maabara yetu Kuu ya Taifa, Hivyo sasa jumla ya wagonjwa wa COVID-19 nchini ni 19,” amesema Waziri Ummy.

Akitoa ufafanuzi wa wagonjwa hao, Waziri Ummy amesema mmoja mwanaume mwenye umri wa miaka 49 alipata maradhi hayo baada ya kukutana na raia wa kigeni aliyetoka nchi zilizoathirika zaidi. Wakati mwingine ni mwanamke mwenye umri wa miaka 21.

“Mwingine ni mwanaume mwenye umri a miaka 49, Mtanzania ambae pia ni miongoni mwa watu waliokuwa wakifuatiliwa,” amesema Waziri Ummy.

https://youtu.be/1O7efG1q1ns

Waziri Ummy amesema kazi ya kufuatilia watu wote wa kjaribu waliokutana na wagonjwa hao inaendelea, na kuwataka wananchi kuchukua tahadhari zaidi juu ya mamabukizi ya ugonjwa huo.
Wakati Tanzania ikitangaza kwamba ina wagonjwa 19, Rwanda mpaka sasa wana jumla ya wagonjwa 70.
error: Content is protected !!