Tuesday , 5 December 2023
Home Kitengo Maisha Afya Wagonjwa mil 1.3 wa corona wapona duniani
Afya

Wagonjwa mil 1.3 wa corona wapona duniani

Spread the love

WAGONJWA 1,394,965 kati ya 4,030,053 waliokuwa wameambukizwa virusi vya corona (COVID-19) wamepona ugonjwa huo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Ugonjwa huo ulioanzia mji wa Wahun nchini China mwishoni mwa mwaka 2019, umesambaa mataifa mbalimbali dunia na hadi leo Jumamosi tarehe 9 Mei 2020 saa 7.50 mchana umesababisha vifo vya watu 276,498.

Kwa mjibu wa mtandao wa Worldmeter inaonyesha hadi muda huo wagonjwa ni 2,358,590 kati yao 2,310,087 sawa na asilimia 98 wanaendelea vizuri huku 48,503 sawa na asilimia 2 wako katika hali mbaya.

Mtandao huo unaonyesha Marekani ndiyo taifa linaongoza kwa kuwa na maambukizi mengi yanayofikia 1,322,164 huku vifo vikiwa 78,616 na wagonjwa 223,749 wakipona.

Hispania inashika nafasi ya pili dunia ikiwa na wagonjwa 260,117. Kati yao wagonjwa 26,299 wamefariki dunia 168,408 wakipona.

Italia ina wagonjwa 217,185 ambapo vifo ni 30,201 na wagonjwa 99,023 wamepona. Uingereza ina wagonjwa 211,364 huku vifo vikiwa 31,241.

China ambako ugonjwa ulianzia, maambukizi ni 82,887 na vifo vikiwa 4,633 huku waliopona 78,046.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari Mchanganyiko

Majaliwa aipongeza GGML mapambano dhidi ya Ukimwi

Spread the loveWaziri Mkuu Kassim Majaliwa ameipongeza Kampuni ya Geita Gold Mining...

AfyaHabari Mchanganyiko

GGML waungana na Biteko kuanika mbinu za mapambano dhidi ya Ukimwi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

AfyaMichezo

GGML yatoa milioni 17 kung’arisha ATF Marathon

Spread the loveKATIKA kuendelea kuunga mkono jitihada za Serikali kukabiliana na maambukizi...

Afya

‘Ambulance’ yawarejeshea tabasamu wananchi Mkuyuni

Spread the loveWananachi wa  Tarafa ya Mkuyuni, Halmashauri ya Morogoro mkoani Morogoro,...

error: Content is protected !!