October 2, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wagonjwa 254 wakutwa na Corona Kenya

Mutahi Kagwe, Waziri wa Afya Kenya 

Spread the love

UGONJWA  wa virusi vya corona (COVID-19) umeendelea kushika kasi nchini Kenya baada ya wagonjwa wapya 254 kuripotiwa. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Taarifa iliyotolewa leo Jumatano tarehe 24 Juni 2020 na Wizara ya Afya ya Kenya imesema, walipima sampuli za watu 4,859 ndani ya saa 24 zilizopita na kubainika 254 kuambukizwa.

Imesema idadi ya walioambukizwa imefikia 5,206.

Waliopona ugonjwa huo wamefikia 1,823 baada ya wagonjwa 41 kuruhusiwa kutoka hospitalini ndani ya saa 24 zilizopita.

Vifo vimeongezeka na 130 kutokana na wagonjwa wawili kufariki dunia ndani ya saa 24 zilizopita. Idadi ya sampuli zilizopimwa tangu ugonjwa huo uliporipotiwa nchini humo miezi takribani mitatu iliyopita imefikia 146,537.

Kwa mujibu wa mtandao wa Worldometer unaonyesha maambukizo ya COVID-19 duniani yamefikia milioni 9.39, waliopona wakiwa milioni 5.09 huku vifo vikiwa 480,579.

error: Content is protected !!