September 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wagonjwa 23 wa corona waongezeka Z’bar

Spread the love

WIZARA ya Afya Zanzibar imetangaza wagonjwa wapya 23 wa Homa Kali ya Mapafu, inayosababishwa na Virusi vya Corona (COVID-19). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa hiyo imetolewa leo tarehe 19 Aprili 2020, na Hamad Rashid Mohammed, Waziri wa Afya Zanzibar, imeelwza kuwa ongezeko hilo linaifanya Zanzibar kuwa na wagonjwa 58.

Amesema wagonjwa wawili kati ya wagonjwa wapya 23, walifariki nyumbani kabla ya kuchukuliwa vipimo. Na kupelekea idadi ya vifo visiwani humo kufikia vitatu.

“Kati ya wagonjwa wapya, 21 wanaishi Unguja na wawili Pemba. Kati yao 21 ni raia wa Tanzania na wawili raia wa kigeni (Cuba na Ufaransa) wanaishi Zanzibar,” amesema Mohammed.

Mohammed amewahimiza wananchi kuchukua tahadhari za kujikinga na ugonjwa huo, ikiwemo kuosha mikono kwa maji tiririka na sabuni.

“Wizara inaomba wale wote wenye dalili za homa kali, kukohoa na kupiga chafya kujitokeza katika vituo vya afya au kupiga namba 190. Ni vyema mgonjwa mwenye dalili za maradhi haya asijichanganye na wagonjwa au watu wengine.

“Na tuache tabia ya kujitibu wenyewe kwani kwa kufanya hivyo tutaendelea kueneza maambukizi na vifo vinavyo husiana na ugonjwa huo,” amesema Mohammed.

error: Content is protected !!