Sunday , 5 February 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Wagombea urais watukanana hadharani
Kimataifa

Wagombea urais watukanana hadharani

Spread the love

 

WAGOMBEA urais nchini Nigeria wamemaliza kampeni zao huku kila mmoja akitoa wito wa kukamatwa kwa mwenzio na wakishtumiana kwa kashfa za zamani za ufisadi. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

“Wewe mgonjwa wa Parkinson, fisadi”; hayo ni baadhi ya maneo ambayo wagombea wawili wakuu katika uchaguzi wa urais nchini Nigeria wametoleana.

Siasa za Nigeria zinakabiliwa na shutuma za kila aina, hasa kuhusu masuala ya pesa zinazopatikana kwa njia haramu.
Waliopendekezwa katika uchaguzi wa urais unaotarajiwa kufanyika tarehe 25 Februari 2023 – ni Bola Tinubu na Atiku Abubakar wote wanaidawa matajiri.

Zaidi ya Wanigeria milioni 93 watashiriki kupiga kura kumchagua mrithi wa Rais Muhammadu Buhari, ambaye hatogombea baada ya kutimiza mihula miwili.

Taifa hilo lenye watu wengi zaidi barani Afrika linakabiliwa na changamoto nyingi, hususan ukosefu wa usalama unaokaribia kuenea nchi nzima, mzozo mkubwa wa kiuchumi na ukosefu wa usawa unaoendelea.
Katika siku za hivi karibuni, wakati kampeni zikishika kasi, matusi na shutuma zimepamba moto baina ya wagombea.

Mgombea wa chama tawala (APC), Bola Ahmed Tinubu hivyo anamshutumu Atiku Abubakar, wa upinzani (PDP), kwa kuendesha biashara ya uhalifu na kujenga himaya kwa njia ya udanganyifu kwa kuiba fedha za umma kati ya mwaka 1999 na 2007, wakati alipokuwa makamu wa rais.

Tinubu, aliyepewa jina la utani la ‘Godfather’ au hata ‘The Boss’ kwa ushawishi na utajiri wake mkubwa, anatoa wito kwa mpinzani wake kujiondoa katika kinyang’anyiro cha urais na kujisalimisha kwa vyombo vya sheria.
Anamuita Abubakar ‘muuzaji wa rasilimali za umma’ kwamba akimtaja ni ‘mfisadi’.

Uchunguzi wa Bunge la Seneti la Marekani unataja jina la Abubakar katika kesi ya utakatishaji fedha.

Kati ya mwaka wa 2000 na 2008, mmoja wa wake zake wakati huo, ambaye ana uraia wa Marekani, anadaiwa kumsaidia mumewe kurejesha zaidi ya dola za Marekani milioni 40 za fedha zinazotiliwa shaka na Marekani kupitia akaunti za nje ya nchi.

Wanandoa hao pia wanatuhumiwa kupokea zaidi ya dola za Marekani milioni mbili kwa kandarasi na kampuni ya kimataifa ya Siemens, ambayo ilikiri hatia katika kesi hii.

Tinubu anatuhumiwa kuwa, katika ujana wake, alipokuwa mhasibu nchini Marekani, aliiba pesa kwa niaba ya mtandao mkubwa wa ulanguzi wa heroini, jambo ambalo anakanusha.

Akiwa na umri wa miaka 70, mgombea wa APC, gavana wa zamani wa Lagos, mara kwa mara amekuwa akishutumiwa kwa rushwa, bila kuhukumiwa.

Timu ya Atiku pia inataka kukamatwa kwa Tinubu, anayetuhumiwa kuandaa ‘jeshi la majambazi’ kudhoofisha uchaguzi huo.

Afya ya wagombea urais ni suala nyeti nchini Nigeria, ambapo Rais Buhari alizua gumzo kubwa kwa kutohudhuria kwa miezi kadhaa wakati wa muhula wake wa kwanza kutafuta matibabu nchini Uingereza kwa ugonjwa usiojulikana.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Papa Francis kukutana na wahanga wa vita Sudan Kusini

Spread the love  KIONGOZI wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis leo Jumamosi...

Kimataifa

Polisi ahukumiwa kifo kwa kumuua wakili

Spread the love  MAHAKAMA kuu nchini Kenya imemhukumu kifo Ofisa wa Polisi,...

Kimataifa

Hospitali za China zilifurika wagonjwa, wazee kipindi cha wa likizo ya Mwaka Mpya wa Lunar

Spread the loveHOSPITALI  nchini China zimejaa wagonjwa na wazee katika kipindi cha...

Kimataifa

Papa Francis ayataka mataifa ya nje kuacha kupora mali DRC

Spread the love  KIONGOZI wa kanisa Katoliki Papa Francis, ameyataka mataifa ya...

error: Content is protected !!