January 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wagombea urais Afrika ya Kati wagomea matokeo

Spread the love

ANDRE Kolingba na Martin Ziguele ambao ni wagombea urais kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati wamegomea matokeo.

Wagombea hao wametaka kuhesabiwa upya kura wakidai kwamba matokeo ya duru ya kwanza ya uchaguzi huo uliofanyika mwezi uliopita, hayana uhalali.

Katika matokeo hayo Kolingba alishika nafasi ya tatu ambapo Ziguele alishika nafasi ya nne. Hata hivyo wamesema kuwa zoezi la kuhesabu kura lilikuwa na kasoro nyingi hivyo kuna kila sababu ya kurejea kuhesababu kura hizo.

Wagombea hao ambao ni wanachama wa muungano wa kisiasa wa AFDT wamewasilisha kesi katika Mahakama ya Katiba nchini humo, kupinga matokeo hayo.

Tume ya Uchaguzi ya nchi hiyo ilitangaza kuwa uchaguzi wa rais umeingia kwenye duru ya pili baada ya kukosekana mgombea aliyepata zaidi ya nusu ya kura zote.

Kwenye uchaguzi huo, walioonekana kupana alama za juu zaidi ni mawaziri wakuu wawili wa zamani wa nchi hiyo ambao ni Anicet Georges Dologuele aliyepata asilimia 24 na Faustin Touadera aliyepata asilimia 19 ya kura zote.

Kwa mujibu wa matokeo hayo Dologuele na Touadera watachuana kwenye duru ya pili itakayofanyika mwishoni mwa mwezi huu.

error: Content is protected !!