Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Wagombea CCM watishiwa nyau Dodoma
Habari za Siasa

Wagombea CCM watishiwa nyau Dodoma

Spread the love

MCHAKATO wa kumpata Naibu Meya wa Manispaa ya Dodoma ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), umeanza huku wagombea waliojitokeza katika kinyang’anyiro hicho wakionywa kutokujihusisha na vitendo vya rushwa, anaandika Mwandishi Wetu.

Akizungumzia mchakato huo, Katibu wa CCM wilaya ya Dodoma, Pili Mbanga, amesema mchakato huo umeanza baada ya Mkurugenzi wa Manispaa hiyo kuwaandikia barua ya kuwasilisha jina la mgombea.

“Mchakato huu ndani ya chama utamalizika ndani ya wiki hii kwa kuwa maelekezo ya Mkurugenzi jina linatakiwa kuwasilishwa Agosti 9, mwaka huu,” amesema Katibu huyo.

Alibainisha hadi sasa wamejitokeza madiwani sita katika kinyang’anyiro hicho akiwemo Naibu Meya wa sasa, Jumanne Ngede anayetetea nafasi hiyo.

Aliwataja wengine ni Msinta Mayaoyao, Ally Mohamed, Abel Shauri, Jakobu Lemanya na Neema Mwaluko.

Aliwataka kutotumia rushwa katika uchaguzi huo kwa kuwa kiongozi mzuri anapatikana bila rushwa.
“Hawatakiwi kutoa au kupokea rushwa na ikibainika ameshinda kwa kutumia rushwa CCM itamuengua,” amesema Mbanga

Kadhalika, Mbanga amesema mchakato wa chaguzi mbalimbali ndani ya chama na jumuiya zake unaendelea na unatarajiwa kukamilika Agosti 5, mwaka huu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

error: Content is protected !!