Zitto Kabwe, kiongozi wa chama hicho ametoa kauli hiyo leo tarehe 6 Septemba 2020, jijini Dar es Salaam akieleza kuwa, kadhia hiyo pia imewakumba madiwani wao.
Zitto amedai “wagombea wetu waliondolewa kwa sababu zisizokuwa na mashiko…, nasema hakuna wagombea basi hakuna uchaguzi.
“Tumeteua jumla ya wagombea 168 Tanzania Bara, lakini mpaka sasa wagombea walioruhusiwa kuendelea na kampeni ni 104 tu. Wagombea 24 wa ACT-Wazalendo wameenguliwa na wasimamizi wa uchaguzi na wengine 24 waliwekewa pingamizi.”
Akizungumzia wagombea wa chama hicho Zanzibar amesema, katika majimbo 50 waliyoweka wagombea, jumla ya wagombea 14 wameeunguliwa na katika hao 14, wagombea tisa wanatoka Pemba.
“Kisiwa cha Pemba kina majimbo 18 pekee, hivyo nusu ya wagombea wetu wameenguliwa na Kisiwa cha Unguja wagombea wetu watano wakienguliwa,” amesema.
Soma zaidi: Zitto ataja kosa la Chadema kwa Lowassa Sumaye
Ametaja baadhi ya sababu zilizochambuliwa na Omar Said Shaaban, mwanasheria wa chama hicho zilizoelezwa na wasimamizi wa uchaguzi ni pamoja na kughushiwa pingamizi kwamba zimetolewa na vyama vingine vya siasa.

“Kule Zanzibar kabla hujagombea, lazima muajiriwa aandike barua na uruhusiwe na muajiri wake, sisi tuna ushahidi wagombea wetu wameandika na walipata ruhusa ya muajiri.
Zitto ametaja sababu zingine ni pamoja na wagombea wao kutopokelewa picha za wagombea na baadaye kuwaengua kwa madai ya kutoweka picha kwenye fomu zao.
Amesema, pingamizi zingine zimebuniwa na ofisi za wasimamizi nje ya sheria, wasimamizi kutokuwepo ofisini, kubadilisha maandishi ya wagombea, wasimamizi wa uchaguzi kukataa baadhi ya wadhamini ilhali wapo kwenye daftari la mpiga kura, pia kukaata mihuri ya mahakama, kufanya uamuzi kabla ya majibu ya pingamizi.
Zitto amesema, mchakato wa rufaa unaendelea na kwamba Mwanasheria Mkuu wa chama hicho anafuatalia kwa karibu ikiwa ni pamoja na kuwsasilisha ushahidi wa usio na shaka kwenye maeneo husika.
Halafu Profesa Kaabudi eti anamuhakikishia balozi wa Uingereza kuwa uchaguzi eti uko shwari na utaendelea bila matatizo. Nyie mnafikiri hao mabalozi hawaelewi? waangalizi pia wanaelewa na wataandika katika ripoti zao