July 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wagombea 11 waenguliwa kugombea urais

Wafula Chebukati, Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka nchini Kenya (IEBC)

Spread the love

 

TUME Huru ya Uchaguzi na Mipaka nchini Kenya (IEBC) imewaondoa wanasiasa 11 kushiriki katika kinyang’anyiro cha urais wa nchi hiyo unaotarajiwa kufanyika tarehe 9 Agosti, 2022 baada ya kushindwa kuwasilisha majina ya wagombea wenza wao kabla ya tarehe 16 Mei, 2022. Anaripoti Mwandishi Wetu… (endelea).

Miongoni mwa walioenguliwa ni pamoja na mgombea wa Chama cha African National Congress, Musalia Mudavadi; Spika wa Bunge la Kitaifa, Justin Muturi na Lengala David William kutoka chama cha Jirani Mzalendo.

Wengine ni Mbugua Mwaura, Kihuha Waringa, Aoko Ongir, Odhiambo Onyango, Ndekerere Kundu, Ngechu Gichuki, Katoni Ndambuki na Nyagoko Oanda.

Akizungumza katika mkutano wa majadiliano na wagombea urais na wawakilishi wao, Mwenyekiti wa IEBC, Wafula Chebukati amesema wagombea hao walitakiwa kuwasilisha majina ya wagombea wenza kabla ya tarehe 16 Mei, ili tume ijiandae vya kutosha kwa uchaguzi huo.

Chebukati amesema majina ya Mudavadi na Muturi yamo kwenye orodha hiyo baada ya kuwasilisha maelezo kuwa wanmuunga mkono Naibu Rais William Ruto.

Chebukati amesema hawataruhusu wagombeaji kuwasilisha majina ya wagombea wenza chini ya miezi mitatu kwenye uchaguzi.

Amebainisha kuwa walikuwa wamehamia kwenye hatua ya kuthibitishwa huku wagombea urais wote wakihitajika kuwasilisha sahihi 2,000 kutoka kwa angalau kaunti 24 kabla ya kuidhinishwa kuwania.

“Mara baada ya tume kumaliza uhakiki wa wafuasi, ambapo kuna upungufu wa saini katika idadi, wanaotaka watapewa muda wa kutosha kupata saini zilizobaki,” amesema.

error: Content is protected !!