August 13, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wageni nchini wapewa angalizo

Spread the love

WAFANYAKAZI wa kigeni wametakiwa kuzingatia kanuni na sheria za kazi hususan vibali vya ajira na ukaazi ili kutokiuka sheria za nchi, anaandika Regina Mkonde.

Hayo yamesemwa na Hilda Kabissa, Kamishna wa Kazi Nchini kwa niaba ya Jenista Mhagama ambaye ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Kazi katika mkutano wa 57 wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE).

“Wageni wanatakiwa kufuata utaratibu sababu unapokuwa huna vibali vyote ni ukiukwaji wa taratibu, kanuni na sheria za kazi,” amesema Kabisa.

Aidha amewataka waajiri kuwapa motisha wafanyakazi wao pamoja na kuwasilisha michango yao katika mifuko ya hifadhi ya jamii ili wanapostaafu wasipate shida katika upataji wa viinua mgongo vyao.

” Watumishi pia wazingatie maadili na taratibu za kazi waache kujohusisha na rushwa,” amesema.

Aggrey Kamukala Mkurugenzi wa ATE amesema kuwa kwenye mkutano huo wadau mbalimbali walojadili mada za utata wa sheria za ajira hasa kwa wageni na kwamba sheria hiyo inatungwa.Pia amesema kuwa changamoto zilizojadiliwa kwenye mkutano huo zitawasilishwa serikalini ili zitungwe sheria ama kuboreshwa zilizopo ili kuondoa changamoto hizo.

” changamoto kweli zipo na ndiyo màana inatungwa sheria mahsusi kwa wageni na itambulike kwamba utungwaji wa sheria ni jambo lingine na utekelezwaji wake vilevile nibhatua nyingine,” amesema.

Amesema vilevile wadau walijadiri sheria ya uratibu wa ajira za wageni.

error: Content is protected !!