July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Waganga wa jadi 18 mbaroni

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Henry Mwaibabe

Spread the love

WAGANGA wa jadi 18, wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Kagera, wakidaiwa kukutwa na nyara za Serikali zenye thamani ya sh. milioni 60.4. Anaandika Mwandishi wetu… (endelea)

Watuhumiwa hao wamenaswa katika oparesheni ya kuwasaka watu wanaojihusisha na vitendo vya mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino) na vikongwe.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Henry Mwaibabe, operesheni hiyo ilianza juzi katika Wilaya ya Biharamulo kwa kuwashirikisha polisi na kikosi cha Maliasili.

Amesema kuwa, watuhumiwa hao walikamatwa katika vijiji vya kata nne za Kabindi, Nyamigogo, Runazi na Nyabusozi tarafa ya Nyarubunga.

Amesema msako huo umeanzia katika wilaya ya Biharamulo kutokana na sehemu hiyo kushamiri kwa vitendo vingi vya kishirikina na mauaji ya albino.

“Tutahakikisha tunapambana kukomesha vitendo vya mauaji ya watu wenye ulemavu kwa kuwakamata watu wote wanaojihusisha na ukatili huo. 

“Tumejipanga kulinda albino na vikongwe, tunaomba jamii iwe tayari kuwafichua wale wote wenye dhamira ya kujihusisha katika vitendo hivyo,”amesema.

Mwaibambe ameongeza kuwa baada ya kukamilika taratibu za mahojiano, watuhumiwa wote 18 watafikishwa mahakamani ili kujibu mashitaka.

Naye Afisa Wanyamapori wa Pori la Burigi, Jimmy Mushana, amesema operesheni hiyo imefanikisha kukamatwa nyara 39 zitokanazo na  wanyama na ndege zenye thamani sh. milioni 60.4.

error: Content is protected !!