July 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Waganda wanaswa na pembe za Ndovu

Spread the love

 

JESHI la Polisi Kanda Maalum Dar es Saalam limewakamata watu wawili Raia wa Uganda wakiwa na pembe 660 za Ndovu pamoja na mashine ya kukatia pembe hizo, anaandika Hamisi Mguta.

Simon Siro, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam amewaeleza waandishi kuwa, watuhumiwa hao ni Juma Saidi (54) na Ally Sharif (26) wamekamatwa Kimara jijini Dar es Salaam.

Watuhumiwa hao wamekamatwa huko Mbezi katika nyumba ya kupanga ambapo ndipo walikokua wakiishi.

Kutokana watuhumiwa hao na wengine mbalimbali kukamatwa wakiwa katika nyumba za kupanga Kamanda Siro amesema ili kuwepo kwa usalama, wamiliki wa nyumba za kupanga waendeleze zoezi la kuwa na picha za wapangaji wao.

“Nafikiri mnakumbuka niliwaambia ili tuwe salama watanzania, unayempangisha hakikisha kwamba unaweka picha yake hiyo itatusaidia kumtafuta na kumkamata pindi anapofanya tukio,”amesema.

Kamanda Siro amesema upelelezi bado unaendelea ili kubalini mtandao mzima wanaoshirikiana nao kufanya uhalifu wa kuua na kuchukua pembe za ndovu.

“Tutahakikisha wanatueleza mtandao wanaoutumia na kisha tutawafikisha  mahakamani kujibu mashitaka yanayowakabili,”amesema.

 

error: Content is protected !!