SHIRIKA la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch linasema, mamlaka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), zilipuuza tahadhari za mara kwa mara za kutokea ghasia katika gereza kuu la Kasapa, mapema mwa mwaka jana. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).
Katika ghasia hizo, kumethibitika kuwa wafungwa wakike 56 walibakwa na wafungwa wenzao wa kiume kwa siku tatu mfululizo.
Mwaka mmoja baadaye ripoti mpya inatoa wito kwa mamalaka za DR- Congo kuchunguza kwa kina kilichofanyika na kuwachukulia hatua waliohusika na unyanyasaji huo.
Uchunguzi unaripotiwa ulianza siku moja baada ya ghasia hizo, lakini mpaka sasa, bado haujakamilika, kutokana na kile kinadaiwa kuwa ukosefu wa rasilimali.
Taarifa zinasema, kati ya wafungwa 56 waliobakwa, wafungwa 37 akiwamo msichana wa miaka 16, wametoa ushahidi mbele ya mwendesha mashtaka wa jeshi wakisema, ni wahanga wa ghasia na ubakaji.
Baadhi ya manusura walibakwa mara kadhaa na wanaume tofauti katika ghasia hizo zilizodumu kwa siku tatu.
Uchanguzi unasema, waathirika saba walipachikwa mimba na wengine kuambukizwa magonjwa ya zinaa ikiwa ni pamoja na virusi vya HIV/Ukwi.
Watafiti wanataka waathirika wapatiwe huduma ya matibabu na msaada wa afya ya akili.
Septemba mwaka jana (2020), wafungwa 2,000 wa gereza kuu la Kasapa walifanya ghasia na kuchoma moto majengo ya gereza hilo na kuwashambulia wafungwa wa kike.
Mlinzi wa gereza alifariki kutokana na majeraha aliyoyapata wakati wa ghasia hizo, na vikosi vya usalama viliripotiwa kuwapiga risasi watu wasiopungua 20 katika vurugu hizo.
Leave a comment