Tuesday , 23 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Wafungwa 600 watoroka jela baada ya shambulio
Kimataifa

Wafungwa 600 watoroka jela baada ya shambulio

Spread the love

 

MAOFISA wa magereza nchini Nigeria wamesema watu wenye silaha walishambulia jela moja katika mji mkuu juzi usiku tarehe 5 Julai, 2022 na kusababisha wafungwa zaidi ya 600 kutoroka. Gereza hilo linawashikilia wahalifu mashuhuri wakiwemo maafisa wa zamani wa serikali na wanamgambo wa kundi la Boko Haram.

Shambulio hilo lilifanyika saa chache baada ya watu wenye silaha kufyatulia risasi msafara wa Rais wa nchini hiyo, Muhammadu Buhari katika jimbo la Katsina alikozaliwa.

Shambulio dhidi ya gereza hilo la Abuja ni tukio la hivi karibuni katika msururu wa mashambulizi mabaya yanayotekelezwa na makundi yenye silaha nchini Nigeria.

Watu wenye silaha nzito walivamia jela hilo Jumanne usiku, kwa kufyatua risasi na kulipua vilipuzi.

Maafisa wamesema askari mmoja wa kulinda gereza aliuawa na wafungwa 600 waliachiwa huru na washambuliaji kabla ya kufurushwa na maafisa wa usalama.

Kulikuwa ulinzi mkali kwenye jela hilo jana Jumatano huku maafisa wakisema wameanza msako wa wafungwa waliotoroka. Maafisa wanasema watoro 300 wamekamatwa tena.

Jumatano, ndugu wa wafungwa walikusanyika kwenye uwanja wa gereza wakitarajia taarifa mpya kutoka kwa mamlaka ya gereza.

Hakuna kundi lililodai kuhusika na shambulio hilo la Jumanne, lakini maafisa wanalishuku kundi la kigaidi la Boko Haram.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!