October 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Wafungwa 4 kati ya sita waliotoroka gerezani wakamatwa tena

Spread the love

 

WAFUNGWA wanne kati ya sita raia wa Kipalestina waliotoroka kutoka jela yenye ulinzi mkali mapema wiki hii huko nchini Israel wamekamatwa. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Kwa mujibu wa taarifa ya polisi nchini Israel imesema, wawili walipatikana katika maegesho ya magari mapema asubuhi ya jana Jumamosi tarehe 11 Septemba 2021.

Wengine wawili walikamatwa karibu na jiji la Nazareti Ijumaa tarehe 10 Septemba 2021.

Msako ulianzishwa Jumatatu baada ya wafungwa hao sita kutoka nje ya gereza la Gilboa kaskazini mwa Israel, tukio la kwanza la kutoroka gereza la Palestina kwa kiwango hiki kwa miaka 20.

Makundi ya wapiganaji wa Palestina wakati huohuo yalisifu kutoroka kwao wakikiita kitendo hicho kuwa cha ‘kishujaa’.

Wafungwa hao waliotoroka wanaaminika kuchimba shimo kwenye sakafu ya gereza lao kwa miezi kadhaa na kuweka shimo kuelekea chini ya gereza.

Wanafikiriwa kutambaa kupitia shimo hilo na kufikia ukuta wa nje wa gereza, kisha wakachimba handaki lililoibuka katikati ya barabara ya udongo, chini tu ya mnara wa walinda usalama.

Picha za CCTV ziliwanasa wakiacha handaki saa 01:30 Jumatatu. Lakini kengele ilipigwa saa 04:00 alfajiri baada ya wenyeji kuripoti kuona watu wanaoshukiwa kuwa wafungwa katika uwanja karibu na gereza.

Vyombo vya habari vya Israeli vimeshutumu kutoroka jela kwa wafungwa hao vikiashiria kuzorota kwa usalama.

error: Content is protected !!