Takriban wafungwa 38 wamefariki dunia na wengine 69 kujeruhiwa katika ajali ya moto ulioteketeza gereza kuu la mji mkuu wa Burundi – Gitega mapema. Anaripoti Mwandishi Wetu.. (endelea)
Moto huo uliozuka mapema leo Jumanne tarehe 7 Disemba, 2021 bado haijabainika ni nini chanzo cha moto huo.
Kwa mujibu wa Makamu wa rais wa Burundi, Prosper Bazombanza ambaye alitembelea kituo hicho na hospitali ambapo wengi wa majeruhi wanatibiwa, amesema 12 kati ya waliofariki walikosa pumzi kwa kuzingirwa na moshi wakati 26 waliosalia walipata majeraha ya moto.
Amewaambia waandishi wa habari kuwa majeruhi 34 waliopata majeraha ya moto ya wastani na zaidi wamepelekwa hospitali huku wengine wakipatiwa matibabu katika eneo la gereza.
“Wafanyikazi wa afya wametuhakikishia kwamba watapona”, alisema. Ameongeza kuwa gharama za matibabu zitalipwa kikamilifu na serikali.
Hali mbaya ya usalama ilifanya iwe rahisi kwa moto huo kuenea haraka katika gereza hilo lenye uwezo wa kubeba watu 400 lakini sasa lilikuwa na wafungwa zaidi ya 1500. Kiwango kamili cha uharibifu kilikuwa bado hakijajulikana.
For CHRISMASS SEASON MORE BOOKS IN WRITING SEASON…….
http://static.booktopia.com.au/pdf/9780857197689-1.pdf