MWENYEKITI wa Chama Cha Wafugaji Tanzania (CCWT) kimesema wakuu wa wilaya wanachangia kwa sehemu migororo ya wafugaji kwa kuchochea ukamatwaji wa mifugo pindi inapoingia kwenye mbuga za hifadhi ya serikali. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma… (endelea).
Hayo yamelezwa Jijini Dodoma leo Jumatatu na Mwenyekiti wa CCWT Taifa, Mrida Mshote Marocho katika mkutano mkuu wa uzinduzi wa kadi za kielekroniki kwa wanachama wa chama hicho.

Mwenyekiti huyo amesema kutokana na uwepo mgogoro kati ya wafugaji na wakuu wilaya, Serikali inaombwa kuona namna bora ya kuwakutanisha wafugaji na wakuu wa wilaya ili kutatua migogoro pale mifugo inapoingia kwenye hifadhi.
Pamoja na mambo mambo mengine ameiomba serikali kuona namna bora ya kutenga na kuboresha maeneo ya malisho ya mifugo sambamba na uboreshaji wa majosho ya kuoshea mifugo.
Akizungumza katika uzinduzi huo Mwenyekiti amesema wafugaji wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na kusumbuliwa kwa ukamatwaji wa mifugo yao.
Amesema hivi karibuni ng’ombe zaidi ya 100 zinashikiliwa na mkuu wa wilaya tunduru mkoamni Ruvuma ahali inayosababisha usumbufu kutokana na kile kinachosadikiwa ni kuingia katika maeneo ya hifadhi.
Katika hatua nyingine kiongozi huyo wa wafugaji amewataka wanachama wa chama hicho kujiandikisha kwa kutumia kadi za kielekroniki ili kuepukana na kutapeliwa.
Kwa upande wake Makamu mwenyekiti wa chama hicho, Busundwa Wamarwa amesema wafugaji wafikirie uwekezaji katika viwanda kwa ajili ya kuongeza thamani ya mifugo yao.
Amesema maeneo mengi ya ufugaji yanakabiliwa na changamoto kubwa ya uhaba wa maji hivyo jambo ambalo ameeleza kutokana na hali hiyo wafugaji wamekuwa wakijikuta wanahamahama.
Pia amesema wafugaji wanatakiwa kuwa na umoja na ufugaji wenye tija na uboreshaji wa maeneo ya malisho na sehemu za unyweshaji wa mifugo.
Kwa upande wake mgeni rasmi katika uzinduzi huo, Naibu Katibu mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Ezron Nonnga amesema kwa sasa serikali imeshanunua mizani 70 kwa ajili ya kupima uzito wa mifugo.
Amesema kuwa utaratibu ambao kwa sasa umewekwa na Serikali ni kuhakikisha mifugo inauzwa kwa thamani ya uzito na siyo kuuzwa kwa makadirio.
Leave a comment