Friday , 3 February 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Wafugaji watishia usalama Shamba la Mtibwa
Habari Mchanganyiko

Wafugaji watishia usalama Shamba la Mtibwa

Spread the love

 

WAFUGAJI wanadaiwa kutishia usalama wa maafisa uhifadhi wa Shamba la Miti la Mtibwa, kufuatia vitendo vyao vya kuvamia kambi zao, kwa ajili ya kupora ng’ombe wanaokamatwa kwa kosa la kuingizwa shambani humo, kinyume cha sheria. Anaripoti Mwandishi Wetu, Morogoro … (endelea).

Taarifa hiyo ilitolewa jana tarehe 10 Juni 2021, mkoani Morogoro na Mhifadhi Msaidizi wa Shamba la Miti Mtibwa, Karimo Mangachi, katika ziara ya ukaguzi wa shamba hilo, iliyofanywa na Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa Misitu Tanzania (TaFF).

Akielezea changamoto hiyo, Mangachi alisema wafugaji hao wameunda vikundi vya wahuni, ambavyo huvamia kambi za wahifadhi, kwa ajili ya kupora ng’ombe hao.

“Askari wakienda katika doria ya kawaida wanafanikiwa kukamata ng’ombe, wale watu wametengeneza vikundi vya wahuni kuja kuvamia maeneo ya kambi,” alisema Mangachi.

Mhifadhi huo wa Shamba la Mtibwa alidai kuwa, vikundi hivyo vinawazidi nguvu askari wa ulinzi wa SUMA-JKT.

“Tangu mwezi wa kwanza hadi leo kumekuwa na matukio ya kuvamiwa zaidi ya 10, kwa changamoto hii imekuwa ni tishio kwa wenzetu tuliowapa jukumu la ulinzi, ambao ni Suma JKT. Wanaonekana kuzidiwa nguvu,” alisema Mangachi.

Mangachi alisema “mfano wiki mbili zilizopita walikamata mifugo kama 200, waliletwa kwenye zizi. Usiku iliingia timu kubwa na kuharasi maeneo ya kambi, kwa lengo la kupora mifugo iliyokamatwa,”

“Sasa wakija hapa wanaingia hadi ndani, wanavunja milango na madirisha, waliingia na kuiba vifaa vya kijeshi vya Suma JKT, walichukua butu za kijeshi na baadhi ya kombati za kijeshi.”

Mangachi alisema , vikundi hivyo vya wahalifu huvamia kambi hizo kwa kutumia silaha za jadi na kufanikiwa kupora ng’ombe hao.

“Jeshi lilifanikiwa kukamata ng’ombe 28, ila wale ng’ombe waliokamatwa majira ya mchana, ilipofika jioni kilikuja kikundi cha watu wahuni na silaha za jadi, waliwashambulia askari waliokuwa eneo hili na kutoka na mifugo,” alisema Mangachi.

Kufuatia changamoto hiyo, Kamishna Mhifadhi Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Prof. Dos Santos Silayo, aliwapiga marufuku wafugaji hao kuingiza mifugo kwenye shamba hilo, huku akionya kuwachukulia hatua watakaobainika kufanya kosa hilo.

“Sisi TFS tutaendelea kutoa kila msaada unaohitajika kwa ajili ya usimamizi wa shamba hili, pia tutashukuru kama bodi yako itaendelea kusaidia upande wa pili, wa kutekeleza umuhimu wa sheria ili wananchi wapate uelewa kuwa hii ni rasilimali ya taifa,”

“ Na hawapaswi kuingia katika maeneo ya misitu na hatua kali zitachukuliwa kadri inavyowezekana,” alisema Prof. Silayo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Ndege ya Precision Air yaahirisha safari kwa hitilafu, nyingine yatua kwa dharura

Spread the love  NDEGE ya Shirika la Precision Air imeshindwa kufanya safari...

Habari Mchanganyiko

NMB yakabidhi vifaa tiba hospitali Mtwara  

Spread the loveBENKI ya NMB Kanda ya Kusini imetoa msaada wa vifaa...

Habari Mchanganyiko

Kasilda Mgeni anasisitiza umoja, ushirikiano Same 

Spread the love  MKUU mpya wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda...

Habari MchanganyikoTangulizi

Hii hapa kauli ya Sheikh mpya mkoa wa Dar

Spread the loveSAA chache baada ya kuteuliwa kukaimu nafasi ya aliyekuwa Sheikh...

error: Content is protected !!