Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Wafugaji kumsaidia Dk. Kigwangalla mgogoro wa Loliondo
Habari za Siasa

Wafugaji kumsaidia Dk. Kigwangalla mgogoro wa Loliondo

Pori Tengefu la Loliondo. Picha ndogo kulia, Dk. Hamisi Kigangwalla, kushoto wakazi wa Loliondo
Spread the love

JAMII ya Wafugaji wa Loliondo, Ngorongoro, mkoani Arusha, wamesema kuanzia sasa watakuwa wa kwanza kutoa taarifa kwa yeyote atakayebainika kuingiza mifugo kwenye eneo la hifadhi kama moja ya juhudi ya kumuunga mkono Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla, anaandika Nasra Abdallah.

Wanayasema haya ikiwa ni siku chache tangu Waziri Dk. Kigwangalla kusitisha operesheni ya kuwaondoa katika eneo hilo kwa ile kilichodaiwa na mamlaka za hifadhi madai kuvamia pori tengefu la hifadhi ya Loliondo na kusababisha kaya zaidi ya 400 kukosa makazi huku ng’ombe 2000 waliokamatwa kufa kwa kukosa malisho na 628 kuuzwa.

Operesheni hiyo ya kuwaondoa wafugaji iliyoendana sambamba na uchomaji maboma, inaelezwa kufanywa na polisi wa Longido wakishirikiana na wale wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti (SENAPA) pamoja na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) huku vitongoji zaidi ya 14 vikiwa vimeathirika.

Chanzo cha mgogoro huo kimetokana na Mamlaka hizo za Hifadhi, kutaka kumega eneo la kilometa 1500 la vijiji vinavyozunguka hifadhi hiyo na kuliingiza katika Pori Tengefu, jambo ambalo lilizua hali ya taharuki katika eneo hilo hadi pale Waziri Dk. Kigwangalla alipoingilia kati kwa kusitisha operesheni hiyo Oktoba 27 mwaka huu, alipofanya ziara wilayani humo.

Akizungumza mara baada ya kutembelea mipaka ya vijiji vinavyopakana na pori hilo, Dk. kigwangalla amesema amelazimika kusitisha operesheni hiyo baada ya kupokea taarifa za ukiukwaji wa sheria za vijiji na uwepo wa minong’ono kwamba serikali iliendesha operesheni hiyo kwa kutekeleza matakwa ya muwekezaji.

“Jambo nililoona linaichafua serikali na Rais (John Magufuli) na nilifanya hivyo sababu najua kuna Kamati ya Waziri Mkuu inashughulikia suala la mgogoro wa pori hili hivyo sikuona sababu ya kuanzisha operesheni wakati bado kuna uamuzi wa suluhu ya mgogoro ipo mezani kwa Waziri Mkuu,” amesema Dk. Kigwangalla.

Mwenyekiti Wa Kijiji cha Ololosokwani, Kerry Dukunyi amesema kwa muda mrefu wananchi wamekuwa wakiishi kama wakimbizi kutokana na mgogoro huo ambapo Dk. Kigwangalla kaweza kuwakomboa.

Dukunyi amesema kutokana na hilo hawana budi kumuunga mkono waziri na kufuata maagizo yote aliyoyatoa kuhusu matumizi bora ya ardhi na kuongeza kwamba yeyote watakayembaini kuingiza mifugo katoka hifadhi wao watakuwa wa kwanza kutoa taarifa badala ya kusubiri askari wa hifadhi kuwakamata.

“Pia kanataka niwaambie wananchi kuwa hatutakuwa tayari kumtetea yoyote atakyeingiza mifugo hifadhini na watakayemkata wamfanye chochote wanachojua kwani ukweli ni kwamba hatutaki kurudi tena kwenye mgogoro ambao uligharimu maisha ya ndugu zetu huku wengine wakibaki na ulemavu wa kudumu kutokana na vipigo walivyokuwa wakivipata wakati wa operesheni,” amesema mwenyekiti huyo.

Mmoja wa wananchi aliyejitambulisha kwa jina la Thomas Kayiruu, amewaonya wale wote wenye nia ya kumdhoofisha waziri na juhudi zake za kumaliza mgogoro huo kwa maslahi yao waache mara moja.

Kayiruu amesema maamuzi ya waziri huyo ni ya kuungwa mkono kwani katambua dhana nzima ya ushirikishwaji wa jamii katika uhifadhi na kuongeza kwamba hakuna mtu kutoka nje atakayekuja kutunza hifadhi zetu bali ni wananchi wenyewe.

“Siku zote wamasai tumekuwa wahifadhi wazuri na ndio maana unaona ni jambo la kawaida wanyama wa porini kuja kwenye makazi yetu bila kutudhuru, hivyo baadhi ya watu wenye maslahi yao wanataka kujenga uadui kati ya wakazi wa eneo hilo na wanyama ambao baadaye wanaweza wakasababisha watu kutoona umuhimu wa kuwepo wanyama katika eneo hilo,” amesema mwananchi huyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

Habari za SiasaTangulizi

Shibuda amlima waraka mzito Bulembo

Spread the loveMKONGWE wa siasa nchini, John Shibuda amemshukia kada maarufu wa...

error: Content is protected !!