July 31, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Wafugaji kuiburuza serikali mahakamani

Spread the love

 

WAFUGAJI kutoka wilaya nane za mkoani Morogoro, wameazimia kuifikisha serikali mahakamani kutokana na kukerwa na zoezi la kupiga chapa na utambuzi wa idadi ya mifugo yao, anaandika Christina Haule.

Zoezi la kupiga chapa mifugo linalotakiwa kufanywa na serikali nchini hivi karibuni na kudai, kitendo hicho kinalenga kuwakandamiza wafugaji na hakina nia njema na maisha yao.

Wakizungumza katika mkutano wa pamoja ulioandaliwa na Chama cha Wafugaji Mkoa wa Morogoro, wafugaji hao wamesema kuwa, wanajiandaa kuipeleka serikali mahakamani kupinga zoezi hilo kutokana na kutokuwa na imani na zoezi linaloendelea katika vijiji vyao.

Kilindi Lestino, kiongozi wa kimila wa wafugaji hao amesema kuwa, wametoa  tamko la pamoja la kupinga zoezi hilo na kwamba, serikali haikupita kutoa elimu kwa wafugaji kabla ya zoezi kuanza.

Kochocho Mgema, Katibu wa Chama cha Wafugaji amesema, ni vema serikali ikatatua kwanza changamoto zinazowakabili wafugaji ndipo waanze kufanya zoezi hilo.

Na kwamba, wafugaji hao wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa sehemu za kulishia mifugo zinazotambulika.

Abdallah Mwanjara, Mwanasheria wa Chama cha Wafugaji amewataka wafugaji hao kutokuwa na hofu kufuatia kesi yao ya kupinga zoezi hilo kuwa katika hatua za mwisho za maandalizi na kwamba, itafunguliwa mapema ili kuweza kupata suluhu ya kujua lengo kuu la serikali ni nini.

Hata hivyo amewataka wafugaji kutofanya maandamano yoyote katika kupinga zoezi hilo kwa madai maandamano sio suluhu hasa katika mambo yanayohusu sheria.

Mkutano huo umefanyika kwa kuwashirikisha wafugaji zaidi ya 800 kutoka katika Wilaya ya Malinyi, Mvomero, Kilombero, Ulanga,Wilaya ya Morogoro na Kilosa.

Serikali kwa sasa iko katika zoezi la utambuzi wa idadi ya mifugo, maandalizi ya zoezi la kupiga chapa mifugo  yote iliyopo katika kila halmashauri kwa lengo la kuzuia uingizaji wa mifugo mipya ili kupunguza migogoro iliyokuwa ikijitokeza mara kwa mara.

error: Content is protected !!