January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wafugaji kuanza kunufaika na mifugo yao

Spread the love

KATIKA kuhakikisha kwamba wafugaji wa Tanzania wanaanza kunufaika na shughuli zao, jopo la wataalamu kutoka Taasisi ya Uchunguzi wa Mifugo Tanzania (TALIRI) wamekutana mkoani hapa kwa siku tatu kwa ajili ya kutunga progamu maalumu ya uzalishaji wa mbegu bora za mifugo Tanzania. Anaandika Dany Tibason, Mpwapwa … (endelea).

Programu hiyo ambayo inalenga kwenye uzalishaji wa mbegu bora na za kisasa za mifugo ya aina zote, unatarajia kuweka mwanzo mpya wa matumaini kwa wafugaji nchini Tanzania.

Kaimu Mkurugenzi wa Chuo cha Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) Mpwapwa, Dk. Daniel Komwihagilo amesema wafugaji wengi wa Tanzania wanatamani kuwa na mbegu bora za mifugo zitakazo wapa viwango vikubwa vya nyama na maziwa.

“Wafugaji wengi nchini hawana mbegu bora za mifugo kwa sababu uzalishaji wa mbegu bora za mifugo ulipungua sana tangu mwanzoni mwa miaka ya 1980.

“Hivyo tunataka tuanze upya kuzalisha mbegu bora na za kisasa za mifugo ili kuwapa wafugaji wa Tanzania fursa ya kuwa na mifugo bora na inayoendana na soko la kimataifa la maziwa na nyama,” alieleza.

Mbali na hilo Dk. Komwihangilo amesema ili nchi iweze kuwa na maendeleo ya kweli ni lazima iwekeze zaidi katika masuala ya utafiti.

Amesema utafiti ndiyo njia pekee ambayo inaweza kuibua mambo mbalimbali ambayo yanaweza kulisababishia taifa kuwa na maendeleo makubwa na ya ufanisi zaidi.

“Kuna kila sababu ya kuwepo kwa fungu la kutosha kwa ajili ya utafiti jambo ambalo linaweza kulifanya taifa kuwa na maendeleo ni kuwekeza zaidi katika utafiti.

“Utafiti ndiyo njia pekee ambayo inaweza kuonesha dira ya maendeleo, kwa sasa siyo kweli kuwa wafugaji hawahitaji mifugo bora na mizuri lakini kutokana na kutokuwepo na utafiti wa kutosha wafugaji wanakosa kile wanachokitana na wakati mwingine wanalazimika kutafuta mifugo bora nje ya nchi,” alieleza Dk. Komwihangilo.

error: Content is protected !!