CHUO cha Cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Kanda ya Kati kimewapatia mafunzo ya unenepeshaji mifugo wafugaji wa Kata ya Mlowa Tarafa ya Makan’gwa wilayani Chamwino mkoani Dodoma, anaandika Dany Tibason.
Mafunzo hayo yanalenga kuwasaidia wafugaji hao kuwa na mifugo bora ambayo pia itaweza kuingia katika ushindani wa soko jambo ambalo watajivunia.
Akizungumza leo katika ufungaji wa mafunzo hayo Dk, Thomas Mwachambi kutoka VETA amesema kuwa, lengo la mafunzo hayo ni kuwasaidia wafugaji wa ng’ombe kuwa na mifugo bora na yenye tija.
Amesema kuwa, wafugaji wengi wamekuwa wakifuga kienyeji hali ambayo imekuwa ikisababisha mifugo hiyo kutokuwa na ubora.
Anifa Byemelwa, Ofisa Tarafa ya Makang’wa amesema kuwa, wafugaji wanatakiwa kubadilika kutoka kienyeji na kuwa wa kisasa ili waweze kuondokana na umaskini.
Diwani wa kata hiyo Adrea Msambazi amesema kuwa, mafunzo hayo yanahitajika katika eneo hilo ambalo lina wafugaji wengi kwani waliopatiwa mafunzo hayo ni wachache.
More Stories
Samia aungana na viongozi Afrika kumpongeza Ruto
Askari 818 wahitimu, wawili watimuliwa chuo cha uhamiaji
Dk. Makakala: Chuo cha uhamiaji chachu maendeleo, usalama