May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wafuasi wa Zuma wamkingia kifua asipelekwe gerezani

Jacob Zuma

Spread the love

 

WAFUASI wa rais wa zamani wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, wamezingira nyumba yake ili kuzuia kiongozi huyo asikamatwe. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Hayo yanafanyika wakati Jumanne iliyopita, tarehe 29 Juni 2021, Mahakama nchini humo, kumhukumu Zuma, kifungo cha miezi 15 gerezani, baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kudharau agizo la kufika mahakamani.

Ni katika kesi inayomkabili ya ufisadi.

Uamuzi huo, ulimtaka Zuma kujisalimisha yeye mwenyewe hadi usiku wa manane, jana Jumapili.

Haijulikani kama uamuzi wa mahakama wa kusikiliza rufaa dhidi ya uamuzi wake wenyewe yanaathiri tarehe ya mwisho iliyowekwa ya Zuma kujisalimisha.

Mahakama ya Katiba ilisema kwamba ilipokea ombi la kukata rufaa ya Zuma Ijumaa na italifanyia maamuzi ya ombi hilo tarehe 12 Julai 2021.

Wakati huo huo, Taasisi ya Jacob Zuma, mfuko wa misaada wa rais wa zamani, ilisema rufaa dhidi ya amri ya kukamatwa itasikilizwa na mahakama kuu ya jimbo la Kwa Zulu-Natal Jumanne.

“Hakuna haja ya mimi kwenda jela leo,” Zuma aliwaambia wanahabari siku ya Jumapili nje ya makazi yake huko Nkandla katika jimbo la Kwa-Zulu Natal.

Amedai amepewa adhabu ya kwenda jela bila ya kusikilizwa na kudai “Afrika Kusini inarejea kwa kasi katika utawala wa kibaguzi.”

Mfuasi wake mmoja, Lindokuhle Maphalala, ameliambia shirika la habari la AFP kuwa kama mkuu wa polisi angekuja kumkamata Zuma “kwanza inabidi aanze na sisi.”

“Makabiliano mabaya yangetokea kama kama polisi wangejaribu kunikamata,” Jacob Zuma aliwaambia mamia ya wafuasi wake ambao walilipuka kwa miluzi na shangwe.

Mkusanyiko huo wa wafuasi wa Zuma ni haramu kwa kuwa unavunja kanuni za kudhibiti ugonjwa wa corona, lakini hakukuwa na askari walioenda kuwaondosha watu. Hali hiyo imewafanya baadhi ya watu kuona kuwa kiongozi huyo yupo juu ya sheria kwa kuwa ana nguvu kubwa ya kisiasa.

Zuma mwenye miaka 79, aliondolewa madarakani mwaka 2018, baada ya miaka tisa madarakani, akikabiliwa na shutuma za ufisadi.

Wafanyabiashara walishutumiwa kwa kula njama na wanasiasa kushawishi mchakato wa kufanya uamuzi.

Watu wanaomuunga mkono Zuma wakiwa katika eneo la makazi la rais huyo wa zamani huko Nkandla tarehe 3 Julai 2021.

Lakini Zuma amerudia kusema yeye ndiye mwathiriwa wa njama za kisiasa. Amekataa pia kutoa ushirikiano katika uchunguzi juu ya makosa wakati wa uongozi wake.

Rais huyo wa zamani alitoa ushahidi mara moja tu wakati wa uchunguzi wa kile kilichojulikana kama “kutekwa kwa serikali” lakini akakataa kujitokeza tena baadaye.

Katika suala tofauti la kisheria, Zuma alikana shutuma zilizomkabili katika kesi yake ya ufisadi iliyohusisha makubaliano ya silaha ya thamani ya dola bilioni 5 kutoka miaka ya 1990.

Umati wa wafuasi wamekusanyika nje ya nyumba yake katika mkoa wa KwaZulu-Natal – wengi wakitarajia kuhakikisha kuwa hapelekwi gerezani.

Mvutano wa kisiasa umekuwa ukiongezeka nchini Afrika Kusini wiki hii, huku wanachama wa chama cha maveterani wa jeshi wakitishia kwamba nchi hiyo italegalega ikiwa Zuma atakamatwa.

Chama tawala cha Afrika Kusini cha ANC, ambacho Zuma alikuwa akiongoza, kimetaka utulivu. Lakini akiogopa mgongano mkutano wa kamati yake kuu ya kitaifa umeahirishwa wikiendi hii.

error: Content is protected !!