May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wafariki dunia wakijipiga ‘Selfie’ kwenye radi

Spread the love

 

WATU 16 nchini India, wamefariki dunia kwa kupigwa na radi, wakati wakijipiga picha ‘Selfie’. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Kwa mujibu wa mitandao hiyo, tukio hilo limetokea jana Jumapili, katika Mji wa Kitalii wa Jaipur Kaskazini mwa India.

Watu hao wanadaiwa kujipiga picha wakiwa juu ya mnara wa saa maarufu mjini humo, wakati mvua inanyesha.

Inaelezwa kuwa, takribani watu 27 walikuwa juu ya mnara huo wakati tukio hilo linatokea, ambapo baadhi yao walifanikiwa kuruka chini.

Mitandao hiyo imeripoti kuwa, watu wengine 12 wamefariki dunia kwa kupigwa na radi ya umeme, katika majimbo ya Uttar Pradesh na Madhya Pradesh.

Jeshi la Polisi nchini humo limesema kuwa, asilimia kubwa ya waliofariki dunia katika mkasa huo ni vijana.

Inadaiwa kuwa, radi huuwa watu 2,000 kila mwaka nchini India.

error: Content is protected !!