Wednesday , 8 February 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Wafanyakazi Yacht Club wambwaga mwajiri wao mahakamani
Habari Mchanganyiko

Wafanyakazi Yacht Club wambwaga mwajiri wao mahakamani

Wakili kutoka Kampuni ya Mawakili ya CS, Claus Thomas Mwainoma
Spread the love

HATIMAYE mgogoro uliodumu kwa zaidi ya miaka mitano kati ya wafanyakazi wa Kampuni ya Dar es Salaam Yacht Club na mwajiri wao, Brian Fernandes umefikia tamati baada Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) kutoa ushindi kwa wafanyakazi hao wiki iliyopita. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Wafanyakazi hao zaidi ya 49 walifungua kesi hiyo mapema Februari mwaka huu wakimlalamikia Meneja wa kampuni hiyo ambaye pia ndiye mwajiri wao (Fernandes) kuwa ameshindwa kufuata taratibu za ajira kwa mujibu wa Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya mwaka 2004.

Meneja wa Yatch Club, Brian Fernandes

Wafanyakazi hao walikuwa wakilalamikia mambo muhimu matatu ambayo ni unyanyasaji wa mahala pa kazi, kunyimwa haki ya kujiunga na vyama vya wafanyakazi  mathalani TUICO, kutokuwepo kwa Muundo wa utumishi (scheme of service) wa kada husika pamoja na mpango wa mafunzo.

Aidha, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana tarehe 4 Aprili, 2022 kwa niaba ya wafanyakazi hao, Wakili kutoka Kampuni ya Mawakili ya CS, Claus Thomas Mwainoma amesema baada ya mgogoro huo kufikishwa CMA ulisikilizwa kwa njia ya usuluhishi ambapo mwajiri aliitwa Machi 31, 2022.

Alisema mwajiri alikiri kuwepo kwa mapungufu hayo na kufikia muafaka kwa kuahidi mbele ya Tume kwamba atayaondoa hayo mapungufu yote ndani ya siku 90.

“Kwamba atatoa Muundo wa utumishi (scheme of service) wa kada husika, wafanyakazi hawataingiliwa kujiunga na vyama vya wafanyakazi na mambo ya unyanyasaji na tofauti zilizokuwepo hazitokuwepo tena.

“Kwa hiyo mgogoro huo umefikiwa mwisho na Msuluhishi Mvungi akatupatia tuzo ya utekelezaji wa hayo waliyoahidi na endapo hayatotekelezwa ndani ya muda uliopangwa hatua za mbele zaidi zitachukuliwa na tuzo hiyo itatumika kukazia madai yao,” alisema.

Aidha, ametoa wito kwa wafanyakazi na waajiri kuzingatia kanuni na sheria za mahala pa kazi ili kutengeneza mazingira wezeshi kwa pande zote mbili.

Aliongeza kuwa wafanyakazi wanaohisi kutokutendewa haki na mwajiri au kwa namna yoyote wameshindwa kuelewa  kanuni za kazi na sheria ya mahala pa kazi, vyombo vya sheria vipo kwa ajili ya kutetea haki zao.

“Wasione tabu kushtaki au kuuliza kwenye vyombo vya sheria ilikupata ufafanuzi zaidi kama wafanyakazi wa Yatch Club walivyofanya tunaamini suala hili litaenda vizuri na utekelezaji utafanyika kama tulivyokubaliana kwenye usuluhishi,” alisema.

Alisema hali ilivyo sasa ni kwamba wafanyakazi wamepata ari ya kufanya kazi kwa sababu wanaamini waliyoyalalamikia yatatekelezwa.

Kutokana na uamuzi huo, mwandishi wetu alimtafuta bila mafanikio Meneja wa kampuni hiyo ya Yacht Club Brian Fernandes ambaye pia ndiye muajiri.

Hata hivyo, Afisa Rasilimali watu wa kampuni hiyo, Stellah Kimaro aligoma kuzungumzia maamuzi hayo ya CMA na kudai kuwa yeye si msemaji wa kampuni.

Aidha, Makamu Rais wa kampuni hiyo inayojihusisha na michezo ya baharini, Ryan Wienand alijibu kwa kifupi ‘no comment’ kwamba hana maoni yoyote kuhusu uamuzi huo wa CMA.

Wakati aliyekuwa mmoja wa wajumbe wa bodi ya Yacht Club hadi kufikia mwaka 2021, Mark Hurt alijitetea kwamba yeye si mjumbe bodi hiyo kwa sasa licha ya kwamba mgogoro huo ulishughulikiwa na bodi hiyo kwa muda mrefu bila mafanikio.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mawakili waiburuza mahakamani TLS, EALS

Spread the love  WAKILI Hekima Mwasipu na wenzake wawili, wamefungua kesi katika...

Habari Mchanganyiko

Uvuvi bahari kuu wapaisha pato la Taifa

Spread the love  SERIKALI imesema uvuvi wa bahari kuu umeliingizia Taifa pato...

Habari Mchanganyiko

DPP aweka pingamizi kesi ya ‘watu wasiojulikana’

Spread the love  MKURUGENZI wa Mashtaka nchini (DPP), ameweka pingamizi dhidi ya...

Habari Mchanganyiko

Washindi saba safarini Dubai NMB MastaBata ‘Kote Kote’

Spread the loveKAMPENI ya kuhamasisha matumizi ya Mastercard na QR Code ‘Lipa...

error: Content is protected !!