Saturday , 10 June 2023
Home Habari Mchanganyiko Wafanyakazi wa Tigo matatani
Habari Mchanganyiko

Wafanyakazi wa Tigo matatani

Spread the love

WAFANYAKAZI wa Mtandao wa Tigo wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za kudukua taarifa za miamala ya pesa ya wateja kwa nia ya kuwaibia. Anaandika Faki Sosi…(endelea).

Wafanyakazi  hao ni pamoja na Mhudumu wa Wateja (Costumer care) na kiongozi wa timu ya wasajili laini za simu (Time leader) na Mawakala wa TigoPesa  ambapo wameshtakiwa kwa hati tofauti.

Kesi ya kwanza imesomwa leo tarehe 2 Agosti 2019, mbele ya Hakimu Mkazi  Salim Aly na Wakili wa Serikali Mwandamizi,  Wankyo Simon.

Hamis Singa (30), ambaye ni ofisi wa Tigo Babati mkoani Manyara na wengine wane, wamepandishwa kizimbani kwa kosa la kudukuwa taarifa za miamala ya wateja na kutakatisha fedha kiasi cha Sh. 26 Milioni.

Washtakiwa wengine kwenye kesi hiyo ni Jailos Joseph (33), Singa Mnunga (32), Japhet Mkumbo (33) na Omari Abdallah (33).

Wakili  Wankyo amewasomea washtakiwa hao mashtaka ikiwa ni pamoja na kosa la kupanga njama.

Kosa hilo linadaiwa kutendwa na washtakiwa wote kati ya Januari 2018 hadi Julai 2019 kwamba,  walipanga njama za kujingizia pesa kwa njia za udanganyifu.

Shitaka la pili linalowakabili washtakiwa wote inadaiwa kuwa, kati ya Januari 2018 na Juni 2019 Arusha na Manyara, walijipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kupitia kupitia miamala ya simu ambapo wanadaiwa kujiingizia kiasi cha Sh. 26 Milioni kupitia mitandao ya Vodacom na Airtel.

 Shitka la tatu linawakabili watuhumiwa waote ambapo wanadaiwa, kati ya Januari 2018 na Juni 2019 wanadaiwa kusambaza taarifa za uongo ambazo ni ‘Tuma pesa kwenye namba hii’.

Shitaka la nne linawakabili washtakiwa wote kuanzisha na kusambaza ujumbe ambao haujaombwa, ambapo Juni 2018 na Julai 2019 walianzisha na kusambaza ujumbe ambao haujaombwa kupitia simu za mkononi za wateja.

Shitaka la tano linawakabili watuhumiwa wote ni kusambaza ujumbe kwa njia ya simu ambao haujaombwa na wateja.

Shitaka la sita linamkabili mtuhumiwa wa pili (ofisa wa Tigo) kwa kiingilia taarifa za miamala mbalimbali ya wateja wa simu za mikoni, ambapo inadaiwa kati ya  Juni 2018 na Julai 2019 Babati mkoani Manyara, akiwa mwajiriwa wa Tigo, aliingilia kuingia taarifa za miamala  kwenye TigoPesa.

Shitaka la saba ni utakatishaji fedha ambapo watuhumiwa wote, kati ya Juni 2018 na Julai 2019 walitakatisha fedha haramu kiasi cha Sh. 26 Milioni wakijua sio halali.

Hakimu Aly amesema kuwa, watuhumiwa hawataki kujibu chochote kitokana na kushitakiwa kwa sheria ya uhujumu uchumi. Ameahirisha kesi hiyo mpaka tarehe 15 Agosti mwaka 2019 ambapo upande wa mashataka umedai mahakamani hapo kuwa upelelezi wa shauri hilo haujakamilika.

Kesi nyengine imesomwa mbele ya Hakimu Mkazi Agostino Rwezile na Wakili Wankyo ambapo mshitakiwa wa kwanza kwenye kesi hiyo ni Mohamed Abdallah , wa pili Mosses Kilosa, wa tatu Kokubelwa Karashani na wanne Godfrey Magoye na Khalfan Milau.

Shitaka la kwanza ni kula njama ambapo linawakabili watuhumiwa wote ikiwa wanaidaiwa kula njama za kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Shitaka la Pili linawakabili kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu ambapo washtakiwa wote wanadaiwa kujiingizia kiasi cha Sh.20 Milioni kwa udanganyifu mali ya wateja wa tigo.

Shitaka la tatu ni kumiliki mali za serikali kinyume cha sheria ambapo mshitakiwa wa kwanza amekutwa na nguo za askari wa Jeshi la Wananchi (JWTZ).

Shitaka la nne linamkabili mshitakiwa wa tatu Kokubelwa la  kuingilia mfumo wa fedha bila kibali ambapo inadaiwa kuanzia Januari 2018 hadi 2019 akiwa ofisi ya Tigo Shop Mlimani City Dar es Salaam akiwa mwajili wa mtandao wa tigo huduma kwa wateja aliingilia mfumo wa kifedha kwa wateja wa mtandao na kutoa taarifa kwa mshitakiwa wa kwanza Abdallah.

Shitaka la tano linamkabili mshitakiwa wa nne Mgoye ambaye ni wakala wa tigo anatuhumiwa kuingilia mfumo wa kifedha ya wateja bila kibali na kutoa taarifa kwa Abdallah.

Shitaka la mwisho ni utakatishaji fedha haramu ambapo inadaiwa kuwa watuhumiwa wote wanadaiwa kati ya tarehe 1 Januari 2018 na Juni 2019 kutakatisha kiasi cha Sh.20 Milioni ambacho walijua kuwa ni zao la fedha haramu.

Wakili Wankyo ameieleza Mahakama kuwa upande wa mashtaka unatoa taarifa ya nia juu ya maombi ya kuruhusu uchunguzi wa kiupelelezi kwenye mtandao wa tigo kwani awali walionesha nia ya kutotoa ushirikiano.

Hakimu Rwezile ameahilisha shauri hilo mpaka tarehe 13 Agosti mwaka huu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Askari Polisi zaidi ya 100 wapigwa msasa wa udereva kukabiliana na ajali

Spread the love  KATIKA kuhakikisha wimbi la ajali za barabarani zinapungua kama...

Habari MchanganyikoTangulizi

Serikali yakana kuhamisha kwa nguvu jamii ya Kimasai Loliondo

Spread the loveWAZIRI wa Katiba na Sheria nchini Tanzania, Dk. Damas Ndumbaro,...

Habari Mchanganyiko

Tunduma watenga 60 milioni kujenga machinjio ya kisasa

Spread the loveHALMASHAURI ya mji Tunduma Imetenga kiasi cha Tshs Miloni 60...

Habari Mchanganyiko

Bilioni 17 kujenga bandari kavu Tunduma

Spread the loveHALMASHAURI ya mji Tunduma iliyopo wilayani  Momba mkoani Songwe imepatiwa...

error: Content is protected !!