January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wafanyakazi wapewa angalizo

Rais Jakaya Kikwete akiwa meza kuu na viongozi wengine wa serikali na TUCTA

Spread the love

WAFANYAKAZI nchini wametakiwa kujiepusha na baadhi ya wanasiasa ambao wanawatumia kufanikisha matwaka yao ya kisiasa. Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Kauli hiyo ilitolewa na Katibu wa Shirikisho la Vyama huru vya Wafanyakazi Tanzania, TUCTA Mkoa wa Dodoma na Katibu wa RAAWU kanda ya kati, Ramadhani Mwendwa, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya mwenendo wa kisasa.

Mwendwa amesema kuwa wapo wanasiasa ambao wanatumia nafasi zao kuwatumia wafanyakazi kwa kuwanunua ili waweze kufanikisha malengo yao ya kisiasa na badala yake wamekuwa wakitelekezwa.

Mbali na hilo amesema wafanyakazi wasikubali kumchagua mtu ambaye hana sera za kutetea masilahi yao na badala yake wamchague kiongozi ambaye ana uchungu na kada ya wafanyakazi.

Akizungumzia sula la masilahi ya wafanyakazi amesema serikali imefanya kakosa makubwa ya kuboresha masilahi ya wanasiasa na kusahau kada ya wafanyakazi.

Mwendwa alisema kwa sasa amefurahishwa na demokrasia kukua na jinsi kura za maoni zilivyoendeshwa kupitia chama cha Mapinduzi kwani imejionesha wazi kuwa viongozi wengi wanatafuta uongozi kwa kutoa rushwa.

“Uchaguzi wa kura za maoni kupitia CCM umetoa mwanga kamili na kuonesha ni jinsi gani viongozi tulionao wanaingia madarakani kwa kununua uongozi.

“Kutokana na mfumo uliopo ambao umetengenezwa na serikali ni jinsi gani watanzania ambavyo wamezoea kutawaliwa na viongozi ambao wananunua uongozi na wanachi hao wamekubali kununuliwa” amesema Mwendwa.

Kiongozi huto amesema kuna kila sababu ya kubadilisha mfumo na kuwawajibisha viongozi wala rushwa na wazembe kazini tofauti na ilivyo sasa ambapo wabadhilifu wa fedha ya Umma wamekuwa wakilindwa na viongozi wenzano.

Akizungumzia uwiano wa wabunge katika bunge amesema anatamani sana kuona wabunge wa vyama vya upinzani wanakuwa wengi bungeni ili kuondoa jeuri ya Serikali kujiona kila kitu inaweza kufanya na kutumia wingi wao wa kura kufanya maamuzi ambayo yanawatesa watanzania.

error: Content is protected !!