August 15, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wafanyakazi Urafiki wagoma

Spread the love

WAFANYAKAZI wa Kiwanda cha Nguo cha Urafiki, jijini Dar es Salaam leo wamegoma kuingia kwa madai ya kutotekelezwa kulipwa malimbikizo yao nyongeza ya mshahara, anaandika Pendo Omary.

Mgomo huo umeanza asubuhi hivyo kusababisha kusimama kwa shughuli za uzalishaji kiwandani hapo.

Hatua hiyo imesababisha Jeshi la Polisi Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) kufika eneo hilo kuangalia hali ya usalama lakini pia wamekuwa wakiwataka wafanyakazi hao kuendelea na kazi.

Wakizungumza na MwanaHALISI Online, wafanyakazi wa kiwanda hicho wamesema, madai yao ni malimbikizo ya nyongeza ya mshahara kutoka Sh. 80000 hadi Sh. 150,000.

“Mwaka jana Mwezi wa Pili tulishinda kesi ya madai ya nyoneza ya mshahara hivyo tulipaswa kulipwa stahiki zetu. Mpaka sasa malimbikizo hayo hayajalipwa. Hivyo tumeamua kugoma ili kushinikiza malipo yetu,” amesema James Charles, mmoja wa wafanyakazi wa kiwanda hicho.

Tarehe 2 Desemba mwaka jana, aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (sasa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam) alitangaza kukifunga kiwanda hicho hadi 7 Desemba, 2015 yatakapotolewa majibu ya kuridhisha kuhusu changamoto zilizosababisha mgomo.

Makonda alichukua uamuzi huo baada ya kuwepo mgomo kiwandani hapo kwa wiki kadhaa.

error: Content is protected !!