Thursday , 25 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Wafanyakazi saba NMB wahitimu mafunzo ya Mwanamke Kiongozi (FFT)
Habari Mchanganyiko

Wafanyakazi saba NMB wahitimu mafunzo ya Mwanamke Kiongozi (FFT)

Spread the love

JUMLA wafanyakazi wa kike saba wa Benki ya NMB wamehitimu mafunzo Mwanamke Kiongozi yanayoratibiwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE)  yenye lengo la kuwajengea uwezo na kuwaongezea ujuzi katika uongozi ili waweze kumudu nafasi za juu za uongozi. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimkabidhi cheti cha utambuzi, Afisa Mkuu wa Huduma Shirikishi NMB, Nenyuata Mejooli kwa kuwa mdhamini mkuu wa mafunzo hayo ya FFT yanayoratibiwa na ATE.

Mafunzo hayo yaliyopewa jina la Female Future Programme (FFT) na kuratibiwa na ATE kupitia Chuo cha uongozi ESAMI, yalitolewa kwa muda miezi tisa.

Akizungumza katika mahafali ya nane ya programu hiyo yaliyofanyika jana tarehe 10 Machi 2023 jijini Dar es Salaam, Afisa Mkuu wa Huduma Shirikishi wa NMB – Nenyuata Mejooli alisema tangu mafunzo hayo yaanze kutolewa 2016, benki hiyo imeshapata wahitimu 26.

Alisema “NMB imekuwa ikitoa udhamini kwa wafanyakazi wake kushiriki mafunzo haya tangu kuanzishwa kwa programu hii mwaka 2016 na imeshapata jumla ya wahitimu 26.

“Tunaamini kuwa wahitimu hawa wanakuja kuleta mabadiliko makubwa katika uongozi kwenye Benki yetu,” alisema.

Aidha, aliwasihi waajiri wote nchini kufanya mikakati ya makusudi kuruhusu viongozi wa wanawake kujiunga na programu hii na zingine zifananazo na hii, ili kuwajengea uwezo wa kukua na kuingia katika ngazi za juu za uongozi wa mashirika au taasisi zao.

Katika mahafali hayo ambayo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliwatunuku wahitimu 65 vyeti, pia aliitunuku cheti cha utambuzi NMB kwa kuwa mdhamini mkuu wa mafunzo hayo.

Pamoja na mambo mengine Majaliwa alitoa kwa wanawake kujitokeza kwa wingi kushiriki katika programu hiyo kwani imeendelea kuwa na matokeo chanya kwa washiriki na kuleta mabadiliko makubwa kwenye utendaji wao wa kazi na kugusa maisha yao binafsi.

“Pia nitoe rai kwa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) kiendelee kutoa mafunzo haya ya uongozi kwa wanawake pamoja na kuendelea kuwa vinara katika kuhakikisha usawa wa kijinsia unafikiwa maeneo ya kazi,” alisema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

THRDC yaongeza mkataba wa ushirikiano na ABA

Spread the love  MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),...

Habari Mchanganyiko

Rufaa ya Equity Benki, State Oil yakwama

Spread the loveMAHAKAMA ya Rufani, jijini Dar es Salaam, imeshindwa kuendelea na...

Habari Mchanganyiko

Bodaboda waeleza mafanikio mafunzo usalama barabarani

Spread the loveMADEREVA bodaboda katika Jiji la Dodoma wameeleza jinsi mafunzo ya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yaahidi kuendelea kuunga mkono Serikali za Mitaa

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imesisitiza dhamira yake ya...

error: Content is protected !!