Tuesday , 23 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Wafanyakazi PURA waaswa kuongeza juhudi
Habari Mchanganyiko

Wafanyakazi PURA waaswa kuongeza juhudi

Spread the love

 

WAFANYAKAZI wa Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) wameaswa kuendelea kufanya kazi kwa juhudi na uadilifu ili kuiletea tija sekta ndogo ya mafuta na gesi asilia nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu, Morogoro … (endelea). 

Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi la Mamlaka hiyo Mha. Charles Sangweni wakati wa kikao cha nne cha baraza hilo kilichofanyika hivi karibuni mkoani Morogoro.

“Tuna dhamana kubwa ya kuhakikisha shughuli za mkondo wa juu wa petroli zinaleta chachu ya maendeleo kwenye mnyororo mzima wa mafuta na gesi asili nchini, na utendaji wetu kama wafanyakazi ndio utafanikisha hili,” alieleza.

Mhandishi Sangweni aliongeza kuwa ni vyema wafanyakazi wote wakajituma katika kutimiza majukumu yao ya kila siku huku wakiongeza ubunifu ili kuongezea thamani katika kile wanachozalisha.

Baraza hilo limeipitia na kujadili taarifa ya mapendekezo ya kuhamisha fedha kwa mwaka wa fedha 2021/22 pamoja na mpango wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2022/23 kutoka idara na vitengo vya taasisi.

Aidha, baraza limejadili taarifa ya maoteo ya mapato ya taasisi kwa mwaka wa fedha 2022/23, hoja za wafanyakazi na masuala mengineyo yahusuyo utendaji kazi na hali bora kwa wafanyakazi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Watuhumiwa 12 wa kilo 726.2 za dawa za kulevya wafikishwa mahakamani

Spread the love  WATUHUMIWA watatu wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kibaha Mkoani...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari Mchanganyiko

GGML yasisitiza kuendelea kuimarisha afya za wafanyakazi

Spread the loveKAMPUNI ya Geita Gold Mining Limited kwa kushirikiana na kampuni...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

NMB yadhamini Mkutano Mkuu ALAT, kufunguliwa na Samia

Spread the loveBENKI ya NMB, imekabidhi hundi yenye thamani ya Sh. 120...

error: Content is protected !!