July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wafanyakazi Nyanza Road wapaza sauti

Spread the love

WAFANYAKAZI wa Kampuni ya Ujenzi wa Barabara ya Nyanza Road, Dodoma wameiomba serikali kuichunguza kampuni hiyo kwa madai ya kukiuka magizo ya kuwalipa wafayakazi kima cha chini cha Sh. 12,500 kwa siku na badala yake wanalipa Sh. 6000 tu, anaandika Dany Tibason.

Mbali na hilo wameiomba Wizara ya Kazi kuichukulia hatua kampuni hiyo kwa madai ya kunyanyasa wafanyakazi wake sambamba na kutowapa mikataba ya kazi.

Wakizungumza na waandishi wa habari kwa wakati tofauti leo mjini hapa, walisema kuwa kampuni hiyo imekuwa ikiwalipa mishahara kinyume na sheria ya kazi inavyoelekeza katika kima cha chini.

Philipo Daniel amesema kuwa, amefanya kazi katika kampuni hiyo kwa zaidi ya miaka minne na amekuwa akilipwa Sh. 4,000 hadi Sh. 6,000 kwa siku kinyume na sheria za nchi zinavyoelekeza katika suala la mishara kwa kima cha chini ambapo wanatakiwa kulipwa Sh. 12,500 kwa siku.

“Wizara ya kazi ilitoa muongozi wa sisi kulipwa Sh.12,500 kwa siku wale wa kima cha chini lakini hawa jamaa wanatulipa Sh.6,000 kwa siku kinyume na agizo la serikali,”amesema Daniel.

Amesema kuwa, kero kubwa ambayo wamekuwa wakikabilina katika kampuni hiyo ni kunyimwa likizo au ruhusa wakati ambapo wanakuwa wagonjwa.

“Wanacho angalia wao ni wewe kuwepo kazini, usipokuja hata kama unaumwa siku yako haihesabiwe, hata kama ukiwa uliumia ukiwa kazini hakuna atakayekufuatailia,”amesema.

Abdalah Mkuruzi, opareta wa mashine amesema kuwa, wamekuwa wakifanya kazi bila kuwa na vifaa vya usalama katika maeneo ya kazi.

“Kila siku tunachana nguo zetu, hakuna hata mtu anayestuka kutununulia vifaa vya kufanyia kazi hali inayochangia kwa kiasi kikubwa kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi,”amesema.

Amesema serikali inatakiwa kulifanyia kazi suala hilo ili kuweza kuwasaidia wafanyakazi hao kupata haki yao ya msingi.

Alipoulizwa juu ya tuhuma za wafanyakzi hao, Meneja Mradi wa kampuni hiyo aliyejitambulisha kwa jina moja na Clishna amesema kuwa, hafahamu chochote na hayuko tayari kutoa ufafanuzi juu ya madai ya wafanyakazi hao.

error: Content is protected !!