July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wafanyakazi Mtibwa Sukari watinga kwa Pinda

Sehemu ya shamba la miwa la Mtibwa

Sehemu ya shamba la miwa la Mtibwa

Spread the love

KATIKA kupinga kinachoitwa “ukatili wa mwekezaji”, wafanyakazi wa Kiwanda cha Sukari Mtibwa mkoani Morogoro, wanakusudia kutinga bungeni kufikisha kilio chao kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda. Anaandika Bryceson Mathias … (endelea).

Hatua hiyo ni baada ya uongozi kuandika barua Na.C.1/18//2015 ya 22/3/2015 iliyosabazwa kwa wakuu wa Idara wa kapumpuni hiyo, Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi mashambani na Kilimo Tanzania (TPAWU) na mbao za matangazo.

Barua hiyo inawataka wafanyakazi wajaze fomu ya kufanya kazi kwa malipo ya kuchelewa kuanzia Mei hadi Juni mwaka huu, na wasiotaka kujaza fomu hizo wajaze likizo bila malipo ili wafanye shughuli zingine.

“Hatua za kututaka tujaze fomu hizo kuanzia 26/03/2015 na kurudisha ofisini kabla ya 1/4/2015 saa mbili, na kwamba mfanyakazi ambaye hatajaza kati ya fomu hizo ndani ya siku tano atakuwa amejifukuzisha kazi, ni ukatili,” alisema mmoja wa wafanyakazi hao.

Kufuatia Tangazo hilo lililosainiwa na Kaimu Meneja Rasilimali, V.T Mazengo na Meneja Mkuu wa Kiwanda cha Mtibwa, Hamad Yahaya, wafanyakazi hao wamesema kuwa hawaridhiki nalo na kwamba baada ya kikao wameamua kutinga kwa Pinda bungeni.

Katika msafara huo wa watu watano, wamo mwenyekiti na mjumbe wa TPAWU, Mwenyekiti wa Vyama viwili vya Wakulima Wadogo wa Miwa ya Nje (MOA) na (TUCCOPRICOS) na mkulima mmoja.

Mapema kabla ya uamuzi huo, wafanyakazi hao walipiga kambi kwenye lango la mwekezaji kudai malipo na mishahara ya Desemba 2014 na Februai 2015.

Pamoja na Naibu Waziri wa Maji aliye pia Mbunge wa Mvomero, Amos Makalla kumtaka mwekezaji awalipe, hakutekeleza agizo hilo, hatua ambayo wafanyakazi na wakulima wanaona amefirisika na kutaka serikali iwapelekee mwekezaji mpya.

error: Content is protected !!