January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wafanyakazi METL wagoma

Spread the love

WAFANYAKAZI wa kiwanda cha kuzalisha mafuta na sabuni, Eastcoast Oil & Fats LTD iliyopo chini ya Mohamed Enterprise LTD, wameshinikiza Afisa rasilimali watu wa kampuni hiyo, Erick Bubelwa afukuzwe kutokana na utawala wake mbovu katika mgomo wao ulioanza leo asubuhi. Anaandika Hamisi Mguta … (endelea).

Akizungumza na MwanaHALISI Online, Mwenyekiti wa chama cha wafanyakazi katika kampuni hiyo (TUICO), Daudi Issa amesema kuwa baada ya mgomo huo kusimamisha shughuli za uzalishaji, viongozi walimtoa nje afisa huyo hivyo wanasubiri kukamilisha ushahidi wake leo na kesho kisha watamuita katika kikao cha kamati ya nidhamu ili kutolea maamuzi.

“Mimi nipo likizo lakini nimefika hapa baada ya kupigiwa simu kuwa wafanyakazi wamegoma kwasababu hawamtaki HR kutokana na kukosa maelewano na wafanyakazi na kuwa na.majibu mabaya.” amesema Isaa na kuongeza

“Tutalichukulia hatua haraka iwezekanavyo ili kazi ziendelee kama kawaida na kila mtu apate haki yake ya kujielezea, na kuhusu mkataba hilo limeshajadiliwa kinachosubiriwa ni kusaini tu ambapo zoezi hilo lilipangwa kufanyika, kwa bahati mbaya wafanyakazi wamegoma kabla halijafanyika.”

Katika mgomo huo, wafanyakazi walikusanyika na kushinikiza kiongozi huyo atolewe kisha kusimama getini na kusababisha kusimama kwa kazi kwa masaa kadhaa wakimshutumu kuwa hajari wafanyakazi badara yake anasimama sana kutetea upande wa wamiliki kuliko wafanyakazi.

Mmoja wa wafanyakazi hao aliyejitambulisha kwa majina ya Jofrey Sadara amesema uongozi wa kampuni hiyo uwapa ahadi za uongo mara nyingi wanapodai masuala.mbalimbali ikiwemo kuongezewa mishahara pamoja na kutoa mikataba kwa wafanyakazi.

Sadara amesema kuwa uwamuzi wa kufanya mgomo huo umetokana na ukimya wa afisa mwajiri ambaye amepewa jukumu la kuwasimamia wafanyakazi hao kushindwa kuwatetea kila wanapodai haki zao za msingi.

Naye mfanyakazi mwengine aliyekataa kujitambulisha jina kutokana na sababu binafsi amesema kuwa suala la mfumo wa uchukuaji fedha kwa wafanyakazi unawabana na kupelekea kufanya kazi bila kupewa malipo yao kwa siku husika.

Akifafanua kiasi wanacholipwa kwa siku, mtoa taarifa huyo amesema kuwa vibarua wa utengenezaji wa sabuni hulipwa 7500 kwa siku huku wafanyakazi wa Boila ni shilingi 8500 hadi 9400.

error: Content is protected !!