July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

‘Wafanyakazi jiungeni na TUICO’

Spread the love

CHAMA cha Wafanyakazi wa Viwanda, Biashara, Taasisi za Fedha, Huduma na Ushauri (TUICO) Morogoro kimeshauri wafanyakazi kujiunga nacho ili waweze kupata utetezi utakaowasaidia kupata maslahi yao, anaandika Christina Haule.

Mgasa Chimola, Katibu wa TUICO Mkoa wa Morogoro amesema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari na kwamba, wapo wafanyakazi ambao hukimbilia TUICO baada ya kupata matatizo na baadaye kushindwa kusaidiwa kutokana na kutokuwa wanachama.

“Tunawapokea wafanyakazi wanaokuja kutaka kutetewa huku wakiwa hawajajiunga, lakini tunawashauri kujiunga kwanza halafu tunawasaidia, kwa nini ungoje tatizo likufikie!, jiunge” amesema katibu huyo.

Amesema, TUICO ipo kwa ajili ya kusaidia wafanyakazi kwa kuwatetea kwenye mambo mbalimbali ikiwemo maslahi yao wawapo kazini na hata watakaposimamishwa kazi au kustaafu.

Amewataka waajiri kujenga urafiki na kufanya kazi na viongozi wa TUICO wa matawi na kuacha kuwa maadui kwani wote wanamtetea mtu mmoja ambaye ni mfanyakazi.

Amesema, chama hicho kimefanikiwa kuongeza idadi ya wanachama kutoka wanachama 3029 mwaka 2011 hadi kufikia 6902 mwaka 2015.

error: Content is protected !!