August 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wafanyakazi Exim wachangia matibabu mtoto mwenye matatizo ya moyo

Spread the love

 

Kaimu Mkurugenzi Idara ya Fedha Benki ya Exim Bw Issa Rajabu (kushoto) akikabidhi msaada wa fedha taslimu kwa Muhasibu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKIC), Mohamed Isimbula ikiwa ni mchango wa wafanyakazi wa benki hiyo ili kusaidia matibabu ya moyo kwa mtoto John Selemani (aliebebwa na mama yake) kutoka mkoani Tanga wakati wafanyakazi hao walipomtembelea mtoto huyo hospitali hapo jijini Dar es Salaam leo

Kaimu Mkurugenzi Idara ya Fedha Benki ya Exim Bw Issa Rajabu (wa tano kushoto) akitoa la faraja kwa wazazi wa mtoto John Selemani (aliebebwa na mama yake) pamoja na uongozi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKIC)  baada ya kukabidhi mchango huo. Wengine ni wafanyakazi wa benki hiyo.

Afisa Muuguzi Msimamizi wa wodi ya watoto Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKIC)  Bi Theresia Marombe (Kulia) akielezea huduma zinazotolewa na taasisi hiyo kwa wafanyakazi wa benki ya Exim walipomtembelea na kutoa msaada wa fedha kwa mtotoJohn Selemani anaepatiwa matibabu kwenye kituo hicho.

Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya Exim wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKIC) pamoja na wazazi wa  mtoto John Selemani walipomtembelea na kutoa msaada wa fedha kwa mtoto huyo  anaepatiwa matibabu kwenye kituo hicho.

error: Content is protected !!