Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Wafanyakazi Benki ya Exim wasafisha magari ya wateja, wagawa zawadi
Habari Mchanganyiko

Wafanyakazi Benki ya Exim wasafisha magari ya wateja, wagawa zawadi

Spread the love

BENKI ya Exim Tanzania imeungana na watoa huduma duniani kusherehekea wiki ya Huduma kwa Wateja huku ikiahidi kuendelea kuwa karibu zaidi na wateja wake kupitia huduma zenye ubunifu zaidi  kwenye soko la huduma za kifedha. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Katika kuthibitisha hilo maofisa waandamizi wa benki hiyo wakiongozwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo, Jaffari Matundu leo tarehe 5 Oktoba, 2022 walishuhudiwa wakiwaongoza wafanyakazi wengine wa benki hiyo kufanya matukio mbalimbali kwa ajili ya wateja wao.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim, Jaffari Matundu (wa tano kulia) na maofisa waandamizi wa benki hiyo wakiwa tayari kusafisha magari ya wateja wa benki hiyo waliofika kupata huduma kwenye tawi la makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam mapema hii leo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja.

Matukio hayo ni pamoja na kufisha magari ya wateja mbalimbali waliofika kupata huduma kwenye tawi la makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam mapema hii leo.

Akitoa salamu za heri kwa wateja na wafanyakazi wa benki hiyo jijini Dar es Salaam wakati wa zoezi hilo, Matundu alisema pamoja na jitihada za benki hiyo kuvutia wateja wapya kupitia huduma mbalimbali za kisasa zinazoeandana na mahitaji ya wateja hao, benki hiyo pia imekuwa ikiweka msisitizo mkubwa katika kuwahudumia wateja wake waliopo.

“Wiki ya Huduma kwa Wateja imetoa tena nafasi nzuri kwa benki kusherehekea jukumu muhimu ambalo tumekuwa tukilifanya kila siku yaani kuwahudumia wateja wetu  na kuonyesha umuhimu wa ushirikiano baina yetu kama uongozi, wafanyakazi pamoja na wateja wetu,’’ alisema.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim, Jaffari Matundu (kulia) akipokea zawadi kutoka kwa wafanyakazi wa benki hiyo wakiongozwa na Mkuu wa Idara ya Huduma kwa Wateja wa benki hiyo, Frank Matoro (katikati) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja.

Kwa upande wake Ofisa Mkuu Idara ya Fedha, Shani Kinswaga alipongeza wafanyakazi wote wa benki hiyo akisema utoaji bora wa huduma ni kiungo muhimu katika kuhakikisha wateja hao wanaridhika huku akiwataja wafanyakazi hao kama mashujaa muhimu ambao wamekuwa wakihakikisha wateja wanaridhika kupitia huduma bora wanazozitoa.

“Zaidi pia ningependa tuendelee kuzingatia na kujitolea katika kutoa huduma bora kwa wateja wetu ambao wameendelea kuwa waaminifu kwetu pia.” alisema Kinswaga wakati akihimiza timu ya wafanyakazi hao kujisikia fahari kwa michango yao.

Katika maadhimisho hayo, mbali na zoezi la uoshwaji wa magari ya wateja ilishuhudiwa wakuu wa Idara mbambali wa benki hiyo wakiwahudumia kifungua kinywa wateja mbalimbali waliofika kwenye baadhi ya matawi ya benki hiyo sambamba na kujadili pamoja maswala muhimu ikiwemo namna bora ya uboreshaji wa huduma za benki hiyo pamoja na kujadili  fursa zinazopatikana kupitia ukuaji wa biashara.

Huku akisisitiza kuwa kila siku ni siku ya huduma kwa wateja katika benki hiyo, Mkuu wa Idara ya Huduma kwa Wateja wa benki hiyo, Frank Matoro alisema benki imeendelea kujitolea kutoa kiwango cha huduma zenye ubora wa hali ya juu kwa wateja wake na wadau bila kujali hali zao au wapi walipo kote nchini.

“Kama sehemu ya hatua za kurejesha fadhila na uaminifu wa wateja wetu, wiki hii yote tumekuwa na shughuli kadhaa za kipekee na maalum  kuonyesha namna tunavyowathamini wateja. Baadhi ya shughuli ni pamoja na kutembelea wateja kwa kushtukiza na kuwazawadia kama njia ya kuwashukuru kwa kuwa waaminifu kwetu.,’’ alisema

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim, Jaffari Matundu (kulia) akifurahia pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja.

Wakizungumzia mapokezi hayo pamoja huduma za benki hiyo baadhi ya wateja wa benki hiyo Bw Hamisi Kozzy kutoka Kampuni ya Business Index pamoja na Bw Rashmit Lathigara kutoka kampuni ya Vin Mart waliipongeza benki hiyo kwa huduma zake za kisasa na zinazoendana na mahitaji yao.

“Kuridhika kwetu na huduma zinazotolewa na Benki ya Exim ndiko kunatufanya tuendelee kupata huduma zetu kupitia benki hii. Ni matumaini yetu kwao kwamba ari hii haitapungua na tupo tayari kupokea mambo mazuri zaidi kutoka kwao,’’ alisema Kozzy.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

error: Content is protected !!