October 21, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Wafanyakazi Benki Ya EXIM wakabidhi msaada kwa Watoto yatima

Spread the love

Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Exim Tanzania wakiongozwa na Meneja Mkuu wa Kitengo cha Mikopo wa benki hiyo Bi Gisela Swai (Kulia) wakikabidhi msaada wa mahitaji muhimu ikiwemo magodoro, mashuka, sabuni na vyakula kwa Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Watoto wetu Tanzania kilichopo eneo la Goba, jijini Dar es Salaam Bw Evans Tegete (Kushoto) wakati wafanyakazi hao walipotembelea kituo hicho mwishoni mwa wiki ili kufurahia pamoja na watoto hao.

 

Meneja Mkuu wa Kitengo cha Mikopo wa benki ya Exim Tanzania hiyo Bi Gisela Swai (Kulia) akikabidhi msaada wa mahitaji muhimu ikiwemo magodoro, mashuka, sabuni na vyakula kwa Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Watoto wetu Tanzania kilichopo eneo la Goba, jijini Dar es Salaam Bw Evans Tegete (Kushoto) wakati wafanyakazi wa benki hiyo  walipotembelea kituo hicho mwishoni mwa wiki ili kufurahia pamoja na watoto hao.

Meneja Mkuu wa Kitengo cha Mikopo wa benki ya Exim Tanzania Bi Gisela Swai (Kulia) pamoja na Afisa Mikopo wa benki hiyo Bi Shida Thomson (Kushoto) wakipata chakula cha mchana pamoja na watoto wa kituo cha kulelea yatima cha Watoto wetu Tanzania kilichopo eneo la Goba, jijini Dar es Salaam wakati wafanyakazi wa benki hiyo  walipotembelea kituo hicho mwishoni mwa wiki ili kufurahia pamoja na watoto hao.

 

Wafanyakazi wa benki ya Exim Tanzania wakiwahudumia chakula na vinywaji watoto wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Watoto wetu Tanzania kilichopo eneo la Goba, jijini Dar es Salaam wakati wafanyakazi wa benki hiyo  walipotembelea kituo hicho mwishoni mwa wiki ili kufurahia pamoja na watoto hao.

 

Asanteni sana! Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Exim Tanzania wakiongozwa na Meneja Mkuu wa Kitengo cha Mikopo wa benki hiyo Bi Gisela Swai (wa pili kulia) wakiwa kwenye picha ya pamoja na watoto wa kituo cha Watoto wetu Tanzania kilichopo eneo la Goba, jijini Dar es Salaam pamoja na  Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho Bw Evans Tegete (wa pili kushoto) mara baada ya kukabidhi msaada wa mahitaji muhimu ikiwemo magodoro, mashuka, sabuni na vyakula kwa uongozi wa kituo hicho wakati wafanyakazi hao walipotembelea kituo hicho mwishoni mwa wiki ili kufurahia pamoja na watoto hao.

Karibuni wageni! Wafanyakazi wa benki ya Exim Tanzania wakiwasili kwenye viunga vya kituo cha kulelea watoto yatima cha Watoto wetu Tanzania kilichopo eneo la Goba, jijini Dar es Salaam wakiwa wamebeba mahitaji muhimu kwa ajili ya kituo hicho ikiwemo magodoro, mashuka, sabuni na vyakula.

Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Exim Tanzania wakiongozwa na Meneja Mkuu wa Kitengo cha Mikopo wa benki hiyo Bi Gisela Swai (kushoto) wakiimba na kufurahi pamoja na watoto wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Watoto wetu Tanzania kilichopo eneo la Goba, jijini Dar es Salaam mara baada ya kukabidhi msaada wa mahitaji muhimu ikiwemo magodoro, mashuka, sabuni na vyakula kwa uongozi wa kituo hicho wakati wafanyakazi hao walipotembelea kituo hicho mwishoni mwa wiki ili kufurahia pamoja na watoto hao.

error: Content is protected !!