Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Wafanyakazi Azam wafariki ajalini
Habari MchanganyikoTangulizi

Wafanyakazi Azam wafariki ajalini

Spread the love

WAFANYAKAZI watano wa Azam Televishen kati ya saba leo tarehe 8 Julai 2019, wamepoteza maisha kwenye ajali iliyotokea katika eneo la Malendi, Wilaya ya Iramba mkoani Singida. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Kwenye ajali hiyo, watu watatu wamejeruhiwa. Akizungumza kuhusu tukio hilo, Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Singida, Sweetbeart Njewike amesema, ajali hiyo imetokea saa 2 asubuhi baada ya gari lao aina ya Coaster kugongana na lori.

“Ni kweli ajali imetokea majira ya saa 2 asubuhi, Coaster iliyokuwa inatoka Dar es Salaam kuelekea Mwanza iligongana na Roli lililokuwa linatoka Igunga kwenda Dar es Salaam. Watu saba wamefariki baadhi yao ni wafanyakazi wa Azam TV,” amesema Kamanda Njewike.

Kamanda Njewike amesema, Jeshi la Polisi linaendelea kufuatilia tukio hilo, ikiwemo chanzo cha ajali na majina ya waliofariki, na kwamba baada ya uchunguzi kukamilika watatoa taarifa.

Merichad Magongo, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Igunga amethibitisha kwamba, wamepokea majeruhi watatu wa ajali hiyo.

Wanyakazi wanaotajwa kufariki kwenye ajali hiyo ni Said Haji, Charles Mwandwi, Salim Mhando, Frolence Ndibalema, Silvanus Kasongo. Majeruhi ni Mohamed Mwishehe, Mohammed Mainde na Artus Massawe.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

error: Content is protected !!