July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wafanyabishara kutafuta fursa Comoro

Bandari ya Mji Mkuu wa Comoro wa Moroni

Spread the love

WAFANYABIASHARA 20 kutoka nchini wanatarajiwa kufanya ziara nchini Comoro ikiwa ni sehemu ya kutafuta fursa za uwekezaji. Anaandika Pendo Omary … (endelea).

Ziara hiyo imeandaliwa na kampuni ya Ocean Business Partners kwa kushirikiana na kampuni za Gallery Tours na The Comoros Chamber of Commerce (UCCIA).

Akizungumza na waandishi wa habari jiji Dar es Salaam, Abdulsamad Abdulrahim, Mkurugenzi wa Ocean Business Partners amesema “ziara hiyo itafanyika kwa siku 4 ambapo itaanza 8-11 June mwaka huu, ambapo itajumuisha wafanyabiashara 20 kutoka Tanzania na watano kati yao ni wanawake”.

“Malengo ya ziara hii ni kuhamasisha wafanyabiashara wa Tanzania na Comoro kushiriki katika uwekezaji, kutoa taarifa sahihi kuhusu hali ya uwekezaji na fursa zilizopo ili wawe na maamuzi sahihi katika kuwekeza Comoro,” amesema Abdulrahim.

Ameyataja malengo mengine kuwa ni kukutana na kujadili ni namna gani wanaweza kuendesha shughuli zao na kufikia maendeleo katika sekta mbalimbali na kuhakikisha wajasiriamali wa Tanzania kutoka sekta mbalimbali, wanapata faida kwa kuwajengea uwezo katika sekta zao binafsi na za umma katika uingizaji na usafirishaji bidhaa, biashara na fursa za kibiashara.

“Hii itakuwa ni fursa ya kipekee kwa washiriki kuvuka mipaka na kukutana uso kwa uso na wafanyabiashara wa Comoro kutoka sekta mbalimbali,”ameeleza Abdulrahim.

Aidha, amesema wafanyabiashara hao wanatoka katika sekata za mafuta, gesi, makampuni ya simu, wazalishaji, chakula, usafiri, utalii, ulinzi na wachapishaji.

error: Content is protected !!