July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wafanyabiashara watakiwa kuongeza ubora

Spread the love

WAFANYABIASHARA nchini wametakiwa kuzingatia ushandani wa soko ndani na nje ya nchi, anaandika Dany Tibason.

Mbali na kufanyabiashara za kiushindani, pia wametakiwa kuzalisha zilizo na ubora ili ziweze kukubalika kwa wateja.

Kauli hiyo ameitoa leo na Modester Mbuguni ambaye ni mtoa mada kwenye semina ya wafanyabiashara wa Mkoa wa Dodoma na taasisi za kifedha kwenye semina ambayo imedhaminiwa na Kituo cha Utangazaji cha Radio cha AFM, Dodoma.

Katika semina hiyo Modester amesema, wapo wafanyabiashara wengi ambao wamekuwa hawafanikiwi katika biashara zao kutokana na kutokuwa na uwezo wa kuzalisha bidhaa bora.

“Hatuwezi kuendelea kulalamika kwa kukosa masoko ya nje hapa ni lazima mfanya biashara ujitambue na kujiuliza kama biashara yako unayoifanya ina kiwango kiasi gani.

“Lakini lazima ujiulize biashara yako umeitangaza kwa kiasi gani kwa wateja wako na inaweza kuingia katika soko la kimataifa, wapo wafanyabiashara ambao wanafanya biashara ya ubabaishaji haina hata kiwango na mbaya zaidi hawezi hata kuitambulisha.

“Ukifanya biashara ambayo una uhakika nayo na ina ubora wa kiwango cha juu, ni wazi kuwa utapata wateja wengi wa ndani na nje ya nchi,” amesema Mbuguni.

Meneja wa AFM, Tatenda Nyawo amesema, kituo hicho kinafikiria kuandaa somo kwa wafanya biashara pamoja na taasisi mbalimbali ili kuwapatia mbinu za kufanya bishara za ushindani.

Hata hivyo, ameiomba serikali kuangalia uwezekano wa kupunguza ushuru kwa vifaa ambavyo vinaingizwa nchini kwa maana ya kutoa huduma za kielimu.

error: Content is protected !!