Thursday , 28 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Wafanyabiashara wapigiwa debe bungeni
Habari Mchanganyiko

Wafanyabiashara wapigiwa debe bungeni

John Magufuli, Rais wa Tanzania akizungumza na wafanyabiashara nchini
Spread the love

MBUNGE wa Viti Maalum, Jesca Kishoa (Chadema) amehoji ni kwanini serikali haioni haja ya kuwasaidia wafanyabiashara kwa kuwapa riba yenye mikopo nafuu ili iweze kukuza biashara zao, anaandika Dany Tibason.

Akiuliza swali la nyongeza bungeni, Jesca alidai kuwa mikopo isiyolipika imekuwa kwa kiwango kikubwa tangu mwaka 1991 huku akidai sababu kubwa ni mbili ambazo ni mazingira magumu ya biashara pamoja na riba kubwa kwa wafanyabiashara hao.

‘’Je Serikali haioni umuhimu wa haja ya kuwasaidia kwa kuwapa riba nafuu ili iweze ‘kustimulize’ biashara zao,’’ alihoji Jesca.

Akijibu Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji amesema kutokana na mabadiliko ya mfumo wa mwaka 1991 ya sheria ya mabenki na taasisi za fedha, Benki Kuu au serikali haiwezi kutoa mweleko au ukomo wa taasisi za fedha.

Awali akijibu swali la Msingi la Mbunge huyo ambalo alihoji kuhusina na licha ya kuwa na benki nyingi kuliko nchi zote Kusini na Mashariki mwa Afrika, Je kwanini wingi huo bado haujaleta unafuu katika tozo za riba.

Akijibu swali hilo, Dk. Kijaji amesema mabadiliko ya sekta ya fedha ya mwaka 1991 yalipelekea serikali kujitoa katika uendeshaji wa moja kwa moja wa shughuli za kibenki nchini ili kuruhusu mfumo wa Soko huria.

‘’Viwango vya riba za mikopo hupangwa kwa kuzingatiwa gharama za upatikanaji wa fedha, gharama za uendeshaji, gharama za bima, sifa za mkopaji na hatari ya mkopaji kutolipa mkopo pamoja na kasi ya mfumuko wa bei,’’ amesema.

Amesema dhana ya uhitaji na utoaji wa mikopo siyo kigezo pekee kinachoweza kupunguza viwango vya riba hapo nchini.

Dk. Kijaji amesema hatari ya kutolipa ni kigezo kikubwa kinachotumiwa na benki kupanga viwango vya riba za mikopo hususan kwa wajasiriamali wadogo.

‘’Uzoefu uliopo sasa unaonesha kuwa benki zinapendelea kukopesha wajasiriamali waliojiunga katika vikundi kuliko mjasiriamali mmoja mmoja ili kupunguza kiwango cha mikopo isiyolipika,’’ amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

error: Content is protected !!