October 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wafanyabiashara wapewa somo la kuepuka migogoro

Spread the love

AFISA masoko wa Jiji la Dodoma, James Yuna ameutaka Umoja wa Wafanyabiashara waendao minadani (UWABIMIDO), kufanya vikao vya mara kwa mara ili kuhakikisha wanatatua migogoro ambayo inaweza kujitokeza na kuvuruga umoja wao. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Ametoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza na viongozi wa Umoja wa Wafanyabiashara wa minadani mkoa wa Dodoma waliokuwa wakikutanika katika maeneo la Barabara ya kumi na moja na kuhamia maeneoya majengo ili kupisha msongamano katika barabara hiyo.

Yuna amesema wafanyabiashara hao wanatakiwa kuhakikisha wanafanya biashara zao kwa kuzingatia mazingira ambayo yanawazunguka ikiwa ni pamoja na kuondokana na migogoro.

Afisa huyo alisema kuwa wafanyabiashara wote wa minadani wanatakiwa kuwa katika eneo moja ambalo litakuwa linajulikana na kuondokana na kukaa katika maeneo ambayo yanasababisha msongamano ambao unaweza kusabaisha ajali kutokana na sehemu kuwa hatarishi.

Katika hatua nyingine Yuna alisema kuwa ili umoja huyo wa wafanyabiashara wa mnadani  uweze kudumu kunahitajika kuwepo kwa vikao vya mara kwa sambamba na kufanya maridhiano ya kweli badala ya kuishi bila kuwa na mapatano.

Pia alisema kuwa ili biashara iweze kustawi wafanyabiashara hao wanatakiwa kufanya biasha kwa njia ya utulivu,amani pamojana kuzitii mamlaka ambazo zipo kwa kufuata maelekezo wanayopewa badala ya kuwa na malumbano kwa mamlaka husika.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa UWABIMIDO, Jeremiah Magawa alisema malengo na maazimio ya kuhamia eneo la Majengo kutoka eneo la Indipendence ni kutoka na eneo hilo kuwa dogo na kusababisha msongamano ambao haukuwa wa lazima.

Kutokana na hilo Umoja huo umeamua kutafuta eneo kubwa ambalo lipo nje ya miundombinu ya barabara na kuondoa msongamano katika eneola awali .

Hata hivyo alisema wanakabiliana na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na kukosekana kwa usafiri kutokana na baadhi ya wafanyabiashara kugoma kutoka eneo lenye msongamano nakuhamia katika eneo ambalo linaonekana kuwa salama.

Kutokana na hali hiyo Mwenyekiti wa umoja huo ameziomba mamlaka za Jiji la Dodoma kuhakikisha wanawaondoa wafanyabiashara waliokataa kuondoka  katika eneoambali si salama kwa wafanyabiashara hao na kusababisha msongamano usiokuwa walazima.

error: Content is protected !!