Saturday , 20 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Wafanyabiashara waliojenga juu ya miundombinu ya maji wapewa saa 24
Habari Mchanganyiko

Wafanyabiashara waliojenga juu ya miundombinu ya maji wapewa saa 24

Afisa masoko wa jiji la Dodoma James Yuna akiwaondoa wafanyabiashara wanaopanga biashara zao kwenye maeneo hatarishi ya kiafya katika soko la Sabasaba
Spread the love

WAFANYABIASHARA katika masoko yote yaliyopo Jijini Dodoma wamepewa saa 24 kuondoa vibanda vyao vya biashara vilivyojengwa juu ya miundombinu inayopitisha maji. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Agizo hilo limetolewa na Afisa masoko wa Jiji la Dodoma, James Yuna alipokuwa akizungumza na wafanyabiashara wa Soko la Sabasaba muda mfupi baada ya kufanya ziara ya kushutukiza iliyowahusisha maofisa wa Mazingira wa Jiji, Ofisa Masoko wa Jiji pamoja na Mhandisi wa Jiji la Dodoma.

Yuna alisema kuwa haiwezekani wafanya biashara wakajenga vibanda juu ya miundombinu ya maji na kueleza kuwa kwa kufanya hivyo wanazuia utendaji wa kazi za usafi kuwa mgumu na kusababisha maji kuzagaa ovyo.

Katika ziara hiyo Yuna alisema kuwa taratibu za soko zinafahamika na kila mmoja amepata nafasi ya kufanya biashara kisheria ikiwa ni pamoja na kutunza miundombinu ambayo inatakiwa kufanyiwa kazi katika mazingira rafiki.

Kutokana na hali hiyo Yuna ametoa siku moja kwa wafanyabiashara wote waliojenga juu ya mitaro au miundombinu ya kupitisha maji katika masoko yote yaliyopo katika jiji la Dodoma kuondoa vibanda vyao mara moja na wasipofanya hivyo uongozi utabomoa vibanda hivyo wenyewe.

Naye Mkuu wa Idara ya Mazingira na Udhibiti wa Taka Ngumu katika jiji la Dodoma, Dickson Kimaro, amesema kuwa kitendo cha wafanyabiashara kujenga juu ya miundombinu ya maji inasababisha kushindwa kufanyika usafi kwa kuwango kinachotakiwa.

Alisema mitaro ya maji inatakiwa kuwa wazi muda wote ili kuweza kubaini ni wapi kunatakiwa kufanyiwa usafi kwa kuondoataka ngumu, lakini kitendo cha kujenga juu ya mitaro ya maji kinapelekea mitaro hiyo kuziba na kusababisha maji kuzagaa ndani ya soko.

“Tumeshuhudia baadhi ya wafanyabiashara wakijenga juu ya mitaro, wakijenga juu ya mitaro inapelekea kushindwa kufanya usafi kwa ufanisi, kwa ushirikiano mkubwa wa afisa masoko na mimi ninataka mitaro yote ya maji kuwa wazi na kwa nia njema tu waliojenga juu ya mitaro waondoke.

“Kwa sasa mvua zinaendelea kunyesha na kamwe hatuwezi kuruhusu hii hali iendelee maji yamezagaa kila kona kutokana na mitaro kuziba na inaziba kwa sababu ya nyie mmekuwa mkitupa takataka katika mitaro na kuifanya izibe jambo ambalo siyo sawa.

“Lazima masoko yetu yawe safi hakuna sababu ya kufanya biashara katika masoko ambayo ni machafu ikumbukwe kuwa kwa sasa mvua zinaendelea lakini kama haitoshi dunia inakabiliwa na janga la ugonjwa hatari wa corona na ilikushinda magonjwa hayo ni lazimatuzingatie usafi wa mahali tulipo na tunapofanyia shughuli zetu,” alisema Kimaro.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Gardner Habash wa Clouds Fm afariki dunia

Spread the loveALIYEKUWA mtangazaji wa kipindi cha Jahazi kinachorushwa na kituo cha...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

error: Content is protected !!